Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (Mb.) kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mohamoud Thabit Kombo (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway hapa nchini Mhe. Tone Tinnes, katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Wakati wa mazungumzo yao, viongozi hao wamejadili namna ya kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Norway na Tanzania, ikiwemo utekelezaji wa yatokanayo na Majadiliano ya Kisiasa kati ya Tanzania na Norway yaliyofanyika mwezi Januari 2025, jijini Dar es Salaam.
Aidha, kikao hicho kimekumbushia umuhimu wa Jumuiya ya Wanadiplomasia nchini kuheshimu na kutekeleza yaliyoanishwa katika Mkataba wa Vienna kuhusu masuala ya kidiplomasia wa mwaka 1961.
Vilevile, viongozi hao wamejadiliana kuhusu Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika nchini mwezi Oktoba 2025.
Tanzania na Norway zimekuwa marafiki wa muda mrefu na zina uhusiano wa kidiplomasia tangu mwaka 1964.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...