Rais wa Jamhuri ya Cabo Verde, Mhe. José Maria Pereira Neves amewasili nchini Tanzania leo kwa ziara ya kikazi ambapo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na mzungumzaji mkuu katika Ufunguzi wa Mwaka 2025 wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu utakaofanyika Februari 3, 2025 jijini Arusha.

Rais Neves amepokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ambaye aliambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa.

Kabla ya kuingia madarakani, Rais Neves aliwahi kushika nafasi ya Waziri Mkuu wa Cabo Verde kwa miaka 15.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...