Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia malipo ya shilingi Milioni 800.65 kwa wananchi 429 wa Kata ya Mkange wanaopisha ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki inayojengwa toka Tanga kupita Kata hiyo hadi Makurunge Bagamoyo.

Akizungumza katika mkutano huo na wananchi wa vijiji Vitano vya kata hiyo, Mbunge wa jimbo la Chalinze ambaye pia ni Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ameishukuru serikali kwa kuendelea kutatua kero za wananchi na kumshukuru Mhe. Rais kwa kuridhia fedha hizo zilipwe ili wananchi wapishe ujenzi wa barabara hiyo kwa lengo la kuwaletea maendeleo.

Katika hatua nyingine, ameishukuru serikali kwa matayarisho ya ujenzi wa barabara toka Mandera hadi Saadan ambayo inakwenda kufungua fursa kiuchumi.

Wakizungumza baada ya mkutano huo wananchi wa mkange wameeleza furaha yao na kumshukuru Mbunge wao ambaye siku zote amekuwa akipambana kuhakikisha anatatua changamoto zao.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...