Mkurugenzi wa M-Pesa Tanzania Epimack Mbeteni (kushoto) akimkabidhi zawadi na cheti Thabit Juma Idd (wa pili kutoka kushoto), kuwa wakala aliyefanya vizuri zaidi katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha wa kampuni ya Vodacom kwa kanda ya kati. Viongozi wa kampuni hiyo kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam walitembelea sehemu mbalimbali katika kanda hiyo ili kuongea, kutatua matatizo ya wateja wao papo hapo na pia kuwatambua mawakala waliofanya vizuri zaidi. Hii ikiwa ni adhma yao ya kusogeza huduma karibu na wateja na kuendelea kuwaelimisha kuhusu huduma zao. Kulia ni meneja mauzo wa kampuni hiyo wilaya ya Manyoni Bernard Kombe, akifuatiwa na afisa mauzo wa M-Pesa wa kanda hiyo Musa Kushoka. Tukio hili lilifanyika hivi karibuni wilaya ya Manyoni jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa M-Pesa Tanzania Epimack Mbeteni (kulia) akimkabidhi zawadi na cheti cha Elikira Ezekiel (katikati), kuwa wakala aliyefanya vizuri zaidi katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha wa kampuni ya Vodacom kwa kanda ya kati. Viongozi wa kampuni hiyo kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam walitembelea sehemu mbalimbali katika kanda hiyo ili kuongea, kutatua matatizo ya wateja wao papo hapo na pia kuwatambua mawakala waliofanya vizuri zaidi. Hii ikiwa ni adhma yao ya kusogeza huduma karibu na wateja na kuendelea kuwaelimisha kuhusu huduma zao. Kushoto ni meneja usimamizi thamani ya mteja kutoka Vodacom Daudi Ndovu. Tukio hili lilifanyika hivi karibuni wilaya ya Kondoa, jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa M-Pesa Tanzania Epimack Mbeteni akimkabidhi zawadi na cheti cha kuwa wakala aliyefanya vizuri zaidi katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha wa kampuni ya Vodacom kwa kanda ya kati, Idrisa Omary Kondoa jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa M-Pesa Tanzania Epimack Mbeteni akimkabidhi cheti cha kuwa wakala aliyefanya vizuri zaidi katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha wa kampuni ya Vodacom kwa kanda ya kati, Timoth Ndeji Itigi jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa M-Pesa Tanzania Epimack Mbeteni akimkabidhi zawadi na cheti cha kuwa wakala aliyefanya vizuri zaidi katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha wa kampuni ya Vodacom kwa kanda ya kati, Roman Abed Machinga Complex jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...