Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
WAKAZI wanne wa Kanda ya Ziwa mkoa wa Kagera na Mwanza, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka 49 likiwemo la kujifanya wao ni viongozi mbali mbali kutoka serikalini na kutapeli Sh. Milioni tano
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali Mwandamizi Nura Manja imewataja washtakiwa hao kuwa ni Eradius Rwechungura (43), mfanyabiashara mkazi wa Kiseke Mwanza, Heri Kabaju maarufu kama Babylon (37), Mvuvi mkazi Rwamisheni Kagera, Abdurahim Karugula maarufu kama Obra (42), dereva na anaishi Kahoro Kagera na Eradius Apornary (22), mkazi wa Kashai Kagera
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Beda Nyaki washtakiwa wamesomewa mashtaka 49 kati ya hayo mashtaka 11 ni ya kujitambulisha kwa utambulisho wa mtu mwingine, mashtaka 13 ya kutumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la mtu mwingine , mashtaka 23 ya kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu shtaka moja la kuongoza genge la uhalifu na shtaka la mwisho la utakatishaji fedha.
Mshtakiwa Rwechungura peke yake anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutoa utambulisho usio wake, matatu ya kutumia laini iliyosajiliwa kwa jina la mtu mwingine na mashtaka saba ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu wakati mshtakiwa Kabaju yeye anamashtaka sita ya utambulisho usio wake, mawili ya kusajili laini jina kwa kutumia jina la mtu mwingine na mashtaka 11 ya kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.
Mshtakiwa Karugula anamashtaka matatu ya utambulisho usiokuwa wake, matano ya kutumia laini iliyosajiliwa kwa jina jina la mtu mwingine na mashtaka sita ya kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu huku mshtakiwa Apornary akikabiliwa na mashtaka matatu ya kutumia laini ya simu yenye jina la mtu mwingine mwinigine.
Katika shtaka la kwanza inadaiwa kati ya Oktoba Mosi na Desemba 31,2024 eneo lisilojulikana nchini Tanzania washtakiwa wote kwa pamoja waliendesha genge la uhalifu kwa lengo la kutapeli watu tofauti tofauti na kujiwasilisha uongo kwa watu mbakimbali na kujipatia Sh 5,000,000.
Mshtakiwa Rwechungura anadaiwa kujiwasilisha kuwa ni Ofisa kutoka Idara ya Rasilimali Watu katika Ofisi ya Katibu Tawala Wilaya ya Bukoba kwa Eliberth Kalima na kuwa ni Ofisa kutoka Ofisi ya Mkurugenzi katika Halmashauri ya Kahama mjini kwa Filberth Mashim huku akijua si kweli.
Pia Kaguja anadaiwa wa kujiwasilisha kuwa yeye Ofisa kutoka Mfuko wa Hifadhi wa Jamii PSSSF kwa Anunciata Mwageni pia alijiwasilisha kuwa ni Ofisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili kupata taarifa za muajiriwa Christopher Msemwa pia alidai kuwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe kwa Jesca Kibena.
Aliendelea kudai kuwa Kabuja alijiwasilisha kuwa ni Ofisa Rasilimali watu kutoka ofisi ya Halmashauri ya Njombe mjini kwa Rustica Kayombo na Upendo Nsellu pia alijiwasilisha kama Muweka Hazina wa Idara ya Pensheni kwa Lucas Nzota na kuwa angemsaidia kupata mafao yake huku akijua kuwa si kweli.
Mshtakiwa Rwechungura anadaiwa kujiwasilisha kuwa yeye ni Ofisa Takwimu kutoka Halmashauri ya Tunduma mjini kwa Tupilike Mbwile, ofisa mradi kutoka Halmashauri ya Momba mjini kwa Elistulida Mwakyusa na Ofisa rasilimali watu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe kwa Emmanuela Mwambichi.
Aidha washtakiwa wanadaiwa walikuwa wakitumia laini zilizosajiliwa kwa majina ya Bazil Katono, Happyness Jems, Aziza Ramadhani, Royce Frenki, Sajda Abed, Valence Rwezaula, Ben Mhimbira, Benetson Rwenyagira na Sabitina Ally.
Katika mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu ilidaiwa kuwa washitakiwa walitenda makosa hayo katika maeneo yasiyojulikana nchini kupitia kujiwasilisha kwao kwa uongo walijipatia fedha Sh 5,000,000 kutoka kwa watu mbalimbali waliojitambulisha kwao.
Katika Shtaka la utakatishaji inadaiwa kati ya Oktoba 10 na Desemba 31, 2024 katika maeneo yasiyojulikana nchini, washtakiwa wote walijipatia kiasi cha Sh. Milioni tano huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.
Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu ama kwa kupewa kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi bado haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Februari 14, mwaka huu. Washtakiwa wote wamerudishwa rumande.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...