Na Issa Mwadangala

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Godfrey Chongolo amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kwa kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili na kufuata Kanuni na Sheria za nchi.

Mhe. Chongolo ametoa pongezi hizo Machi 07, 2025 wakati akiwakabidhi vyeti vya sifa na zawadi kwa Wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali waliofanya vizuri zaidi kwa mwaka 2024, tukio lililoenda sambamba na sherehe za Siku ya Familia za Polisi maarufu Police Family Day zilizofanyika Vwawa katika Viwanja vya CCM Wilaya Mbozi Mkoani Songwe ambapi sherehe hizo ziliambatana na michezo mbalimbali kama Mpira wa Miguu, Mchezo wa bao, Draft, Pool table na kuvuta kamba.

Aidha katika mashindano hayo washindi wa michezo hiyo walipewa zawadi mbalimbali ikiwa ni pesa taslimu, medani na makombe ili kuendelea kujenga ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na jamii mkoani humo.

Vilevile, amewataka Wakaguzi na askari waliotunukiwa Sifa na Zawadi kuendelea kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu jambo litakalosaidia kuleta chachu kwa askari wengine kufanya vizuri zaidi.

Pia Mhe. Chongolo amempongeza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe (SACP) Augustino Senga kwa kuwaongoza vyema askari waliochini yake kufanya kazi kwa bidi na kuzingatia haki jambo ambalo limesaidia vitendo vya uhalifu kuendelea kupungua mkoani humo.  










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...