Watumishi wanawake wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) @officiatea Leo tarehe 7 Machi 2025 wametembelea Kituo cha Kulea Watoto Miuji Nyumba ya Matumaini Jijini Dodoma kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani ambayo kilele chake huadhimishwa Machi 8 kila mwaka.

Katika ziara hiyo, wametoa msaada wa bidhaa mbalimbali, ikiwemo chakula vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 1.7 kwa ajili ya watoto 65 wanaolelewa kituoni hapo.

Sr. Hellen, mlezi wa kituo, ameishukuru TEA kwa mchango wao, akisema kuwa kituo hicho hutegemea misaada ya wadau ili kuhudumia watoto wake.

Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala wa TEA, Bi. Alice Lukindo, amesema wanawake wa TEA wameamua kusherehekea siku hii kwa kuleta faraja kwa watoto. "Wanawake tuna wajibu wa kutunza familia na jamii. Leo tumeamua kugusa maisha ya watoto hawa."

✨ Kuadhimisha ni kufanya matendo mema! ✨


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...