MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo,  ameliomba Kanisa la  Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) kumwombea Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na taifa zima kwa ujumla  hasa wakati huu wa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu.

Mpogolo, ameyasema hayo,  alimpomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila,  katika ibada ya maalumu ya kumsimika Askofu  Jackson Malongo,  kuwa Askofu Mkuu  Jimbo la Pwani la  Kanisa hilo.

“Tuendeleee kuliombea taifa letu. Tumuombee  Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, yeye ndiye Amiri Jeshi  Mkuu  na yeye ndiyo kiunganishi  kati ya Tanzania na nchi nyingine duniani,”amesema.

Ameeleza, Rais Dk. Samia,  ndiye mama na  mlezi ambaye  amesimama imara kuhakikisha taifa linasonga mbele.

Mpogolo amesemakatika Wilaya ya Ilala pekee Rais Dk. Samia ametoa sh. bilioni 317  za  maendeleo ambazo zitamaliza changamoto mbalimba zikiwemo za maji na  barabara.

“Tuwaombee watanzania wote, amani  na mshikamano. Mwaka huu  ni mwaka wa uchaguzi Mkuu. Tuweke taifa letu kwenye sala zetu. Tumalize uchaguzi kwa amani na utulivu,”amesema Mkuu huyo wa wilaya.

Aidha  amewataka  waumini wa kanisa hilo  na jamii kwa ujumla kujiandikisha na kuhuisha taarifa zao katika Dafrtari la Kudumu la Wapigakura.

“ Tuwaambie na tuwahamasishe watoto wetu  kwenda kujiandikisha. Wale waliojiandikisha waende kuhakiki taarifa zao,”amesema.

Amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa kanisa hilo na kumpongeza  Askofu Malongo kuwa Askofu Mkuu  Jimbo la Pwani.

“Nakushkuru  Makamu Askofu Mkuu na Askofu Mkuu  kwa kuridhia kumwalika Mkuu wa Mkoa katika ibada hii muhimu.Heshima hii hatuta iweka chini bali tutaiweka juu,”amebainisha.

Awali, Askofu Mkuu wa Jimbo la Pwani la FPCT, Malongo, alisema  kanisa  mama la makanisa hayo  limekuwepo nchini  tangu mwaka 1932.

 Alisema kwa kipindi chote tangu kuanzishwa kwake  hapa nchini kwa uongozi wa  Wamisionari na baadaye wazawa  limekuwa na ushirikiano mkubwa na serikali ya Tanzania.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...