Na Mwandishi Wetu

WAFANYAKAZI  wanawake wa Tume ya Ushindani (FCC) wameungana na wanawake wengine wa Mkoa wa Dar es Salaam kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika Machi 8 ya kila mwaka.

Maadhimisho hayo yamefanyika Viwanja vya Leaders Club wilayani Kinondoni na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ambaye ametumia siku hiyo kutoa pongezi kwa wanawake kwa mchango wao mkubwa katika Taifa kupitia shughuli wanazozifanya katika taasisi za umma na sekta binafsi.

Chalamila amesema kuwa mwanamke ni dira, mjenzi, mbunifu, hivyo wakipewa nafasi katika jamii, watafanya kazi kwa ufanisi na kuleta maendeleo kwa Taifa huku akitoa rai wanawake kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pia amewaomba wanawake kuungana kuupinga mfumo kandamizi ambao unakwamisha maendeleo katika nyanja mbalimbali.“Serikali itaendelea kupinga unyanyasaji wa ukatili wa kijinsia pamoja na mfumo dume ambao umekuwa sio rafiki katika jamii, kwani kuna baadhi ya watu bado wanafanya matendo ya ukatili,” amesema Mhe. Chalamila.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tafiti, Miungano ya Makampuni na Uraghibishi (FCC),Zaytun Kikula amesema kuwa tume hiyo inatambua mchango wa wanawake na kutoa fursa ya kushiriki katika maadhimisho hayo.

Ameongeza wanawake ni jeshi kubwa, hivyo ni fursa kwao kuungana na wanawake wote duniani kuadhimisha siku hiyo muhimu, huku akitaja mfano wa wahandisi wanawake Tume ya Ushindani (FCC) wanaofanya vizuri katika kusimamia majukumu mbalimbali ikiwemo udhibitt wa bidhaa wa babdia sehemu mbalimbali za mipaka ya mipakani.  

Pia amesema wanajivunia utamaduni wa tume kutoa kipaumbele kwa wanawake katika kusimamia kikamilifu udhibiti wa bidhaa mbalimbali pamoja na kuendelea kutekeleza mipango ya kuhakikisha kila mtanzania anapata makazi bidha bora za gharama nafuu.

“Wanawake tunajivunia maadhimisho ya mwaka huu, kwani Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa ushirikiano mkubwa ikiwemo kutoa mikopo ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa wanawake kuendesha maisha yao,” alisema Kikula.

Kwa mwaka huu Maadhimisho haya ya Siku ya Wanawake Duniani, yamebeba kauli kauli mbiu : “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji”.










 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...