Kampuni ya GF Trucks kupitia kampuni ya GF Automobile imeingia makubaliano na  Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali  nchini NaCoNGO   ( The National Council of NGOs)  akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo ,Mujtaba  Karmali alisema katika makubaliano hayo yamelenga kunufaisha pande zote mbili

Wao kama wauzaji wa magari na mitambo waliona kuna haja  ya kuingia makubaliano hayo ya kimkakati kupitia mkataba huo na kufanya mambo mbali mbali ikiwemo kutoa Elimu,Kuwajengea uwezo na uelewa katika nyanja mbalimbali.

Pia Karmali amesema wao wameanza mpango wa kuwapatia mafunzo kazi  kwa vijana wanaomaliza  vyuo mbalimbali mfano , VETA na DIT ili kuwajengea uwezo wa  kufanya kazi na kupata uzoefu kazini, Pia alisema  Makubaliano hayo yatarahisisha kuwafikia Makundi ya vijana  nchi nzima na kuungana na serikali katika mpango wa kuhakikisha vijana wanajengewa uwezo wa kuajiriwa na kujiajiri kwa kupita katika vyuo mbali mbali.

Nae Mwenyekiti wa NaCoNGO , Jasper Makala  ameishukuru Kampuni ya GF Trucks kwa kuonyesha njia kwa makampuni ya Kitanzania kuchangia maendeleo ya Jamii kupitia mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali. Alisisitiza kuwa ushirikiano na makampuni binafsi ya ndani ya nchi ni mbinu mojawapo ya kupunguza utegemezi toka nje ya nchi kuelekea katika uendelevu wa Mashirika.

Mkurugenzi wa Masoko wa GF Automobile ,Mujtaba Karmali na Mwenyekiti wa NaCoNGO nchini Tanzania , Jasper Makala wakionyesha nyaraka baada ya kusaini mkataba kwa ajili ya kushirikiana katika Nyanja mbali mabli ilikwamo utoaji wa Elimu na utaalamu jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Masoko wa GF Automobile ,Mujtaba Karmali (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa NaCoNGO nchini Tanzania , Jasper Makala wakibadilishana nyaraka baada ya kusaini mkataba kwa ajili ya kushirikiana katika Nyanja mbali mabli ilikwamo utoaji wa Elimu na utaalamu jijini Dar es salaam.Wengine ni Katibu wa NaCoNGO ,Adamson Masimba (kushoto) na Kulia ni Afisa masoko wa GF Dianarose

Mkurugenzi wa Masoko wa GF Automobile ,Mujtaba Karmali akisaini makubaliano na Mwenyekiti wa NaCoNGO nchini Tanzania , Jasper Makala kwa ajili ya kushirikiana katika Nyanja mbalimbali ilikwamo utoaji wa Elimu na utaalamu jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa NaCoNGO nchini Tanzania , Jasper Makala akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika Nyanja mbalimabli na kampuni ya GF Automobile ilikwamo utaji wa Elimu na utaalamu jijini Dar es salaam.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...