Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mhe.Mama Mariam Mwinyi ametoa rai kwa wadau mbalimbali kuwasaidia Watoto na Wazee wenye mahitaji Maalum katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mariam Mwinyi amesema hayo alipovitembelea Vituo vya kuwalea Watoto SOS, Mazizini na cha Wazee Welezo kuwapa msaada wa vyakula, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 5 Machi 2025.

Aidha, Mariam Mwinyi ameeleza kuwa ataendelea kuwasaidia zaidi Watoto na Wazee wenye mahitaji Maalum ikiwemo vyakula katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Sikukuu ya Eid.

Mariam Mwinyi amewahimiza Watoto kuwa wenye tabia njema na kufanya ibada katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani .

Halikadhalika Mama Mariam Mwinyi amewasilisha salamu za upendo kutoka kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi katika vituo hivyo.

Naye, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto Zanzibar Mhe.Dkt.Riziki Pembe Juma amemshukuru Mama Mariam Mwinyi kwa kuendelea kuwajali Watoto wenye mahitaji Maalum katika vituo mbalimbali Zanzibar.













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...