Na Belinda Joseph, Songea Ruvuma.


Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Manispaa ya Songea James Mgego, amewakumbusha wenyeviti na wajumbe  wa serikali za mitaa kutenda haki bila kubagua wananchi kwa itikadi zao za kidini na kitamaduni badala yake wafanye kazi kwa kutanguliza masilahi ya wananchi nasio yao binafsi kwani cheo ni dhamana.



Akizungumza wakati wakuhitimisha ziara ya Sekretarieti ya CCM Wilaya Songea Mjini katika kata 21 za Manispaa hiyo leo Machi 23 2025 kwenye shule ya Dkt Emmanuel Nchimbi Kata ya Msamala, Mgego amewataka wenyeviti na wajumbe waliopata ridhaa ya wananchi katika uchaguzi wa mwaka 2024, waende wakatende haki ili kuleta usawa katika jamii.


Amesema katika kipindi chote cha ziara hiyo walijikita kutoa shukrani zao za dhati kwa wanachama na viongozi wa Jumuiya zote na wananchi kwa ujumla, kuendelea kukiamini chama kwa kukipatia ushindi wa asilimia 100 mwaka jana, huku matarajio yao ushirikiano huo huo uendelee hata katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025.



Ameeleza kuwa kila mwanachama wa CCM mwenye mapenzi na chama, anaruhusiwa kugombea nafasi za ubunge na udiwani kasoro nafasi ya urais ambayo nikwa Rais Samia, ambapo amewataka wanachama wakae wajipime wakiona wanatosha basi chama kitawapa nafasi ya kila mtu kugombea nafasi hizo wakati utakapofika.


Mgego amebainisha kuwa katika kila kata asilimia kubwa ilani ya CCM imetekelezwa katika miradi mbalimbali ikiwemo barabara, ujenzi wa shule na vyumba vya madarasa vya kisasa, miradi mikubwa ya maji, pembejeo zakilimo kwa bei nafuu n.k, hivyo wananchi wamesema wanadeni kubwa kwa serikali na zawadi pekee kwa serikali ya awamu ya sita ni kura nyingi za kishindo kwa Rais Samia Suluhu Hassan.


Amehitimisha kwa kuwataka wanachama wa chama hicho kuutumia mwezi huu wa mfungo wa Ramadhani na  Kwarezima, kuendelea kuiombea nchi amani,  kukiombea chama cha mapinduzi pamoja na viongozi wa chama hicho kwaajili ya maendeleo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...