Bohari ya Dawa (MSD), imetunukiwa tuzo ya umahiri wa utoaji huduma kwenye sekta ya Famasi nchini (Award of Service Excellence in Pharmaceutical Sector) kupitia tuzo za mwaka za Tanzania Service Excellence Award 2024, zilizoandaliwa na taasisi ya Charted Institute of Customer Service (CICM)

Tunzo hizo zimetolewa hapo jana na taasisi hiyo katika hafla maalum iliyofanyika katika ukumbi wa Holiday In, jijini Dar es Salaam

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Kaimu Meneja wa Huduma kwa Wateja wa MSD Gendi Machumani amesema kupata tuzo ya utoaji huduma bora katika sekta ya afya inaonyesha jinsi jamii inavyothamini huduma bora zinazotolewa na MSD.

Gendi amesisitiza kwamba hiyo inadhihirisha mabadiliko makubwa ya kitaasisi chini ya Mkurugenzi Mkuu Mavere Tukai, ambapo taasisi imeweza kufanya kazi kwa ufanisi na kutimiza malengo ya kuhakikisha tunaboresha mnyonyoro wa ugavi wa bidhaa za afya nchini.

Ameongeza kuwa tuzo hii inawafanya kuendelea kuwajibika kwa ufanisi na kuhakikisha afya za Watanzania zinalindwa kwa kupeleka bidhaa za afya zenye ubora na gharama nafuu na kwa wakati.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...