Kampuni ya PUMA Energy imeandaa futari maalum Zanzibar, ikikusanya pamoja wateja wake, viongozi wa dini na serikali , na wadau wakuu kwa jioni ya shukrani, mshikamano, na tafakari katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Puma Energy Bi. Fatma Abdallah amesema lengo la futari hiyo ni kuimarisha umoja kwani ushirikiano walionao umesaidia sana kufanikisha biashara zao hapa Zanzibar.
Aidha, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ina matarajio makubwa ya kutanua huduma muhimu zitakazowafikia wananchi kupitia miradi ya uwekezaji inayoanzishwa hapo nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Seif Abdallah Juma amesema lengo la kuwepo miradi hiyo ni kukuza sekta ya huduma na biashara ili kukuza pato la nchi
Kampuni ya Puma Energy Tanzania ni wauzaji wa aina mbali mbali za mafuta ya vyombo vya moto na vilainishi; Imekuwepo Zanzibar tangu mwaka 1994 (wakati huo ikijulikana kama BP Tanzania).

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...