Na John Walter -Hanang'

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, amewataka wenyeviti na watendaji wa mitaa, vijiji na vitongoji kuhakikisha wanawapatia wananchi taarifa sahihi kuhusu mapato na matumizi katika maeneo yao. Pia, amesisitiza kuwa ni wajibu wa viongozi hao kuwafahamisha wananchi juu ya mambo mbalimbali yanayofanywa na serikali ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika maendeleo.

Akizungumza akiwa wilayani Hanang’, ambako anafanya ziara ya kikazi ya siku nne kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza changamoto za wananchi, Sendiga aliagiza kuwa kila mwananchi anapaswa kupata taarifa kuhusu matumizi ya rasilimali za umma.

Aidha, amemuagiza Mkuu wa Wilaya kuhakikisha kuwa wananchi wanapokea taarifa muhimu zinazohusu miradi inayotekelezwa na serikali, ili waweze kufuatilia maendeleo na kutoa maoni yao kwa uwazi.

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wilayani Hanang’ inalenga kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na wananchi wananufaika na huduma zinazotolewa na serikali.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...