Na Mwandishi Wetu.


Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari ( Journalists Accreditation Board- JAB) Bw. Tido Mhando, akiongoza kikao cha kwanza cha Wajumbe wa Bodi hiyo ikiwa ni siku moja baada ya kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi na kukabidhiwa Vitendea kazi ambavyo ni Sera, Sheria na Kanuni.


Kikao hicho kimefanyika leo (Jumanne Machi 4, 2025) katika Ukumbi wa Mikutano wa Bodi uliopo Mtaa wa Jamhuri Jijini Dar es Salaam, ili kupokea na kujadili taarifa za utendaji kazi za Bodi, kupitishwa katika Sheria iliyounda Bodi na Kanuni zake, Hati Idhini na miongozo mbalimbali ya uendeshaji wa Bodi kwa nusu mwaka wa Fedha 2024/2025.


Pamoja na mambo mengine, Bw. Mhando na wajumbe wa Bodi wametambulishwa Sekretarieti ya Bodi, ambapo ametumia fursa hiyo kuipongeza Sekretarieti hiyo kwa kazi iliyokwisha kuifanya tangu Oktoba mwaka 2024 hadi sasa na kuahidi ushirikiano ili kuboresha na kuitendea haki dhamana waliyopewa ya kuongeza thamani ya taaluma ya Uandishi wa Habari.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...