Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na dLab inaendelea kuwawezesha wasichana wenye umri wa miaka 14-18 kwa ujuzi wa STEM kupitia programu ya 'Code Lie A Girl'. Mpango huu umewawezesha zaidi ya wahitimu 3,000 katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Arusha, Dar es Salaam, Mbeya, Dodoma, na Mwanza.
Hafla ya mahafali iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliongozwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis akizungumza na wanafunzi na kuwakabidhi zawadi wahitimu huku akisisitiza dhamira ya Vodacom ya kuwawezesha wasichana kwa ujuzi wa programu (coding) na uvumbuzi. Programu hii pia inahimiza ujumuishi kwa ushirikishaji wa wasichana wenye ulemavu, ikionyesha azma ya Vodacom ya kuziba pengo la kijinsia katika teknolojia ya kidijitali.

Mkurugenzi wa Raslimali Watu kutoka Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa programu ya 'Code Like A Girl' yenye lengo la kukuza uelewa wa wanafunzi wa kike katika masomo ya Sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) ambayo yanafadhiliwa na kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na dLab katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Raslimali Watu kutoka Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis (kulia) akamkabidhi zawadi Mwanafunzi Bless Alexander, mhitimu wa mafunzo ya programu ya 'Code Like A Girl' yenye lengo la kukuza uelewa wa wanafunzi wa kike katika masomo ya Sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) yanayofadhiliwa na kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na dLab katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam
.jpeg)

Hafla ya mahafali iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliongozwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis akizungumza na wanafunzi na kuwakabidhi zawadi wahitimu huku akisisitiza dhamira ya Vodacom ya kuwawezesha wasichana kwa ujuzi wa programu (coding) na uvumbuzi. Programu hii pia inahimiza ujumuishi kwa ushirikishaji wa wasichana wenye ulemavu, ikionyesha azma ya Vodacom ya kuziba pengo la kijinsia katika teknolojia ya kidijitali.

Mkurugenzi wa Raslimali Watu kutoka Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa programu ya 'Code Like A Girl' yenye lengo la kukuza uelewa wa wanafunzi wa kike katika masomo ya Sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) ambayo yanafadhiliwa na kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na dLab katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...