Na Said Mwishehe,Michuzi TV -Mbeya
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema Mkoa wa Mbeya umebeba historia kubwa katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika, hivyo vijana wa mkoa huo wanalojukumu la kuilinda.
Wasira amesema hayo leo alipokuwa akipokewa rasmi mkoani humo katika Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya akitokea mkoani Songwe akiendelea na mikutano ya kuzungumza na wanaCCM pamoja na wananchi.
"Nataka niwaambie hapa Mbeya, Chama chetu ni Chama cha historia, sisi ni muungano wa vyama vilivyoikomboa Tanzania na Afrika kwa ujumla, sisi sio chama cha kawaida.
"Vijana ambao hawaelewi ni kwamba sisi ndio tuliosaidia kuikomboa Afrika. Hapa Mbeya ndipo alipopitia Nelson Mandela, hapa Mbeya ndipo alipopitia Sam Nujoma, na wote walipopita hapa kulikuwa na mzee wetu mwanzilishi wa Chama cha TANU alikuwa anaitwa Mwakangale.
"Na yeye ndiye aliewasindikiza kutoka hapa mmoja baada ya mwengine kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mwalimu Julius Nyerere..." amesema.
Amesema viongozi hao waliokuwa katika harakati za ukombozi wa nchi zao hatimaye walifanikiwa kuwaondoa wakoloni na kuwawezesha Waafrika kuwa huru.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...