Uongozi wa Taawanu Islamic Foundation chini ya Mkurugenzi wake Hajat Zahra Dattani, umefika Msikiti wa Taawanu uliopo Ibosa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na kutoa Sadaka ya Futari kwa Waumini wa Maeneo hayo Mnamo Machi 11, Mwaka huu.

Hajat Zahra akiambatana na Mwenyekiti wa Taawanu Afrika Sheikh Kamugunda
wamefika Ibosa katika Msikiti uliojengwa kupitia ufadhili wao, kwa lengo la kuwatakia Heri ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa Waumini hao wa Kiislam, sambamba na kuwapatia Sadaka ya Chakula ambacho ni Mchele, Unga na Sukari ukiwa ni utaratibu wa Viongozi hao kila ifikapo Mwezi Ramadhani.

Awali wakitoa Salaam kwa Waumini wa Msikiti Taawanu, kabla ya kuwapatia Sadaka hiyo, Viongozi hao wamewakumbusha juu ya Kumcha Mwenyezi Mungu na Kuzingatia lengo la funga (saumu) ikiwa ni sambamba na kutenda yaliyo mema ili wapate Thawabu na heri nyingi hapa Duniani.

Aidha katika muendelezo wa shukrani kutoka kwa Waumini hao, ambao mbali na Sadaka hiyo pia wamejengewa Msikiti pamoja na Kisima cha Maji, wamesema Taawanu kwa Sasa imeendelea kuimarika Kijijini hapo kwa kuvuna Waumini wapya, pia waumini wengine wakiendelea kuhamasika kufanya Ibada na mambo mengine mengi ya Heri.











 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...