Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Ireland, Mhe. Neale Richmond, ametembelea Kitengo cha huduma ya Saratani kwa watoto cha Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Baada ya kutembelea na kujionea kazi zinazofanywa katika Kitengo hicho ,Mhe. Richmond alipongeza juhudi za madaktari na wahudumu wa afya kwa kazi kubwa ya kuhudumia watoto wenye saratani.

Pia, alisifu mchango wa Kituo cha Tumaini la Maisha (TLM) katika kuboresha huduma za afya kwa watoto na kusisitiza dhamira ya Serikali ya Ireland kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta ya afya.

Serikali ya Ireland inatoa misaada ya kifedha na kibinadamu kwa Kitengo hicho kupitia Kituo cha TLM ambacho pia kinatoa huduma za matibabu bure kwa watoto wanaougua saratani.

Katika ziara hiyo Mhe. Richmond aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, ambaye pia anawakilisha Ireland, Mhe. Mbelwa Kairuki, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mhe. Nicola Brennan, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Swahiba Mndeme na maafisa wengine wa serikali kutoka Tanzania na Ireland.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...