Na Mwandishi Wetu
Siku chache baada ya Katibu Mkuu na mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emanuel Nchimbi kufanya ziara katika Jimbo la Masasi, Mkoani Mtwara baadhi ya wakazi wa Jimbo hilo wamekiomba chama hicho kuwapitiaha wagombea wanaotakiwa na wananchi kwa ajili ya kuwaletea maendeleo.
Wakazi hao wamesema kuwa,Jimbo hilo lina changamoto mbalimbali zikiwamo miundombinu mibovu ya barabara, umeme unazimika mara kwa mara hali inayosababisha wafanyabiashara kushindwa kufanya shughuli zao ipasavyo.
Fadhiri Abdalah ni miomgoni mwa wakazi hao ambapo anasema kuwa Jimbo Hilo lina upungufu wa vituo vya kutoa huduma ya afya pamoja na watalaam wa sekta hiyo na vitendea kazi, ukosefu wa maji ya uhakika, upungufu wa madarasa pamoja na walimu na vitendea kazi, jambo ambalo limechangia kuwa nyuma kimaendeleo.
Amesema kuwa, baadhi ya wagombea wanaopitishwa na chama hicho wakishaingia madarakani wanashindwa kutekeleza ahadi zao,jambo linalosababisha wananchi kuendelea kukaa kwenye umaskini.
Wamesema kuwa, kutokana na hali hiyo, chama kinapaswa kuteua mgombea anayekubalika na wananchi na kutekeleza ahadi zake ili akipenda kinyume waweze kumuwajibiaha.
"Mara nyingi wabunge wakishapitishwa hawatekelezi ahadi zao, jambo ambalo linasababisha wananchi kudumaa kimaendeleo, hivyo basi tunaiomba CCM kuwaondoa wasioleta maendeleo na kuwapitisha wanaoweza kutekeleza ahadi zao.
"Chama kisiwaangalie watu usoni, wakishapita wanaturudisha nyuma, tunachokitaka sisi ni mbunge ambaye atakubalika na wananchi na kuleta maendeleo,"amesema Abdalah Fadhiri mkazi wa kata ya Jida.
Ameongeza kuwa, wananchi wanahitaji miundombinu ya barabara, soko la uhakika la korosho, umeme, maji na vituo vya afya Ili waweze kupata huduma muhimu za kijamii.
" Tunaomba chama kisiwapitishe watoa rushwa Kwa sababu wanashindwa kutimiza ahadi zao Kwa wananchi ndomana tunabaki kwenye dimbwi la umaskini,"amesema Fadhiri.
Amesema kuwa,kutokana na hali hiyo,chama kinapaswa kupitisha watu makini wenye uchungu na maendeleo.
Amesema kuwa, mpaka sasa Jimbo la Masasi lina changamoto za miundombinu ya barabara, jambo ambalo limechangia wakulima wa korosho mazao yao kuharibika.
"Kuna baadhi ya maeneo tunayolima.korosho gari haipiti kutokana na miundombinu mibovu ya barabara, hivyo basi tunaiomba CCM kupitisha wagombea watakaotimiza ahadi zao,"amesema.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...