Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

SERIKALI imeiagiza Bodi ya Chai kuhakikisha inakuja na mwelekeo mpya katika sekta ya uzalishaji wa chai,ili kuhakikisha wanapandisha Dola kwenye mauzo ya bidhaa hiyo katika maeneo mbalimbali nje ya nchi.

Hatua hiyo imekuja baada ya serikali kuona sekta ya chai iko nyuma kwenye uzalishaji wa bidhaa hiyo,tofauti na sekta nyingine katika mazao ya chakula na biashara ili hali ina wakulima wengi.

Waziri Bashe ameyazungumza hayo katika Mkutano Mkuu wa wadau wa Tasnia ya chai hapa nchini uliofanyika leojijini Dodoma,

Kutokana na hili,Bashe ametoa siku 14 kwa bodi ya chai kuhakikisha wanaunda timu itakayotengeneza mfumo wa wazi wa biashara kati ya mkulima na viwanda ili kuhakikisha kila kinachofanyika kinaonekana.

Bashe amsema bodi hiyo inapaswa kuunda timu ambayo itajumuisha mkulima,serikali pamoja na sekta binafsi ambayo timu hiyo inapaswa kuhakikisha viwanda,wakukima wanajisajili katika mfumo huo.

Alifafanua zaidi ya kuwa,bila ya kufanya hivyo sekta hiyo ya chai haiwezi kusonga mbele kutokana na kwamba wakulima na wafanyabiashara wote wanafanya kazi zao Kwa kificho.

"Bila ya kufanya hivi hatuwezi kufika mbali kwenye sekta hii ya chai nawasisitiza bodi hakikisheni mfumo wa wazi mtakaoutengeneza viwanda vimejisajili asiyetaka basi afutiwe leseni,"alisema Bashe.

Hata hivyo Bashe amesema anasubiri sheria ndogo ipitishwe ili kukamilisha mchakato wa kuunda mfumo wa wazi ambao utakuwa msaada mkubwa kwenye ukuaji wa sekta ya chai hapa nchini.

"Nasisitiza timu hiyo iundwe kama nilivyoagiza,hakuna sekta ngumu kukutana kama sekta ya tasnia ya chai,"-Bashe.

Katika hatua nyingine Bashe ameitaka bodi hiyo kuwaita wamiliki wa kiwanda cha Watco ili wakae nao mezani ili serikali iweze kukinunua kiwanda hicho,huku akisisitiza endapo watu wa Watco waliuza thamani ya kiwanda hicho aliyenunua atakuwa amekula hasara kwa sababu serikali inakwenda kukichukua.

"Niko tayari kubadilisha maamuzi haya endapo watakuwa rayari kukaa na bodi kuskikiza kile watakachoambiwa,vifunguweni viwanda kama haiwezekani serikali itavichukua viwanda vyote,"- Bashe.

Amesema pia Bodi ya Chai imefanikisha ununuzi wa mashine tatu kati ya saba zilizopangwa kununuliwa mwaka huu wa fedha, hatua itakayosaidia kukabiliana na changamoto ya soko kufuatia kufungwa kwa viwanda vya Mohamed Enterprises Ltd (MeTL) na Marvella.

Bashe amesema kuwa mpaka kufikia Machi 25, 2025, mauzo ya chai yameingizia taifa Sh bilioni 50.25 kuanzia Desemba hadi Machi, kupitia vibali vilivyotolewa na Bodi ya Chai kwa ajili ya kusafirisha nje.

Hata hivyo Bashe amesema Serikali kupitia Bodi hiyo imefanikiwa kufungua masoko ya chai katika nchi za Oman, Qatar, Dubai, Japan na Saudi Arabia huku akisisitiza Kiwanda cha Mponde Holdings kimesaini mkataba na Kampuni ya Mumtaz ya Oman ambapo kuanzia sasa watanunua tani 100 za chai kila mwezi.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...