BABATI, MANYARA.

TIMU ya Polisi Tanzania Jumapili hii Aprili 13, 2025 inawakaribisha Cosmopolitan katika mchezo wa Ligi ya Championship, mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Mjini Babati.

Akizungumza  na Waandishi wa habari, Afisa habari wa timu ya Polisi Tanzania Inspekta Frank Lukwaro amesema kikosi hicho kipo vizuri na wachezaji wana ari na morali ya  kuhakikisha kuwa wanapata alama tatu katika uwanja wao wa nyumbani ili kujihajikishia usalama wa kusalia katika ligi hiyo.

Amesema ligi ya msimu huu imekuwa na ushindani mkubwa lakini kwa upande wao wanaendelea kutoa ushindani ili kusalia na hatimaye kujipanga kwa msimu ujao.

Lukwaro amewaomba mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi ili kuwapa hamasa wachezaji waweze kufanya kazi yao vyema na kupata ushindi.

Mpaka sasa timu ya Polisi ipo nafasi ya 10 ikiwa na alama 31 baada ya kucheza michezo 25.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...