Na MWANDISHI WET

DIWANI wa Kata ya Mabibo, wilayani Ubungo, mkoani Dar es Salaam, Joseph Klerruu, ameishukuru na kuipongeza serikali chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake kwa utekelezaji miradi ya maendeleo yenye thamani ya sh. bilioni 15.2 katika kata hiyo.

Diwani Klerruu amesema utekelezaji huo wa miradi umevunja rekodi katika kata hiyo tangu Tanzania ilipopata uhuru mwaka 1961, ambapo kiasi cha sh. 12,315,000,000 kimeelekezwa katika ujenzi, uboreshaji na ukarabati wa miundombinu.

Klerruu aliyasema hayo, Dar es Salaam, alipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mwaka wa fedha 2020-2025 katika Baraza Maalumu la Umoja wa Vijana wa Chamama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Mabibo.

Ameeleza, kiasi hicho cha fedha kimetumika katika utekelezaji wa miradi katika mwaka huo wa fedha, ikihusisha sekta zotezikiwemo za miundombinu, afya, elimu, maendeleo ya jamii, biashara, masoko, ulinzi na usalama, utawala,michezo na utamaduni.

Amesema miongoni mwa miradi iliyotekelezwa ni ujenzi wa barabara ya lami ya NIT- Madoto Mburahati yenye urefu wa Kilometa 1.8 na taa zake iliyogharimu sh. 8,000,000,000.

“ Aidha tumefanya ukarabati resealing kwa Barabara Mabibo Mwisho- Maungio ya Barabara ya Morogoro na taa zake yenye urefu wa kilometa 1.2 kwa gharama ya sh. 4,000,000,000,”ameeleza Diwani Klerruu.

Diwani huyo amesema Kamati ya Maendeleo ya Kata iliyo chini ya usimamizi wake ilifanikisha ukarabati wa Barabara ya Ushese Kilometa 0.770, Mtaa wa Jitegemee kwa gharama ya sh. 5,000,000 ambapo ukarabati kama huo umefanyika pia katika Barabara ya VINA, Mtaa wa Azimio kwa kiwango hicho hicho cha fedha.

“Pia tumefanya ukarabati wa Barabara ya Msikitini- kwa Mzee Mndenge. Ukarabati umefanyika mara tatu lakini ukihusisha kipande cha Mabibo Sekondari, Zahanati ya Mabibo, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Mwembeni Mtaa wa Mabibo Farasi. Kiasi cha shilingi milioni sitini kimetumika,”ameeleza.

Ameongeza, umefanyika ukarabati wa Kalvati eneo la AMI kwa gharama ya sh.20,000,000, ujenzi wa Kalvati eneo la Kanisa la KKKT MabiboUpogoroni kwa gharama ya sh.18,000,000 na ujenzi wa Kalvati katika eneo maarufu kwa Mzee Likonga Mabibo Farasi kwa gharama ya sh.20,000,000.

“Kubwa zaidi ni ujenzi wa kivuko cha waenda kwa miguu maarufu Kivuko cha Gonzaga kwa gharama ya ya shilingi milioni miamoja na tatu. Pia tumefanikisha ukarabati wa Barabara ya Makutano kwenda kwa Binti Kayenga, Luhanga yenye urefu wa kilometa 1.3 kwa gharama ya shilingi milioni miamoja alizotoa Rais Dk. Samia kupitia mfuko wa Jimbo,”ameekeza Diwani Klerruu.

Diwani huyo alieleza, chini ya Rais Dk. Samia, ujenzi wa Barabara ya Zege yenye urefu wa kilometa 1.87 kutoka TIP TOP, Makutano, Binti Kuyenga inatarajiwa kujengwa kwa gharama ya sh. 2,500,000,000.

“Ujenzi utaanza muda wowote kuanzia sasa chini ya Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam (DMDP) Tuynamshukuru Rais Dk. Samia,”amesema.

Diwani huyo ambaye pia ni Mtaalamu wa Masuala ya Ardhi na Majenzi alieleza kufanyiwa kwa uthamini wa mali za wananchi kupisha ujenzi wa Barabara ya Mwananchi- AMI-Zahanati-Miembeni Mabibo Farasi.

“Kukamilika kwa ujenzi wa barabara hii kutaondoa msongamano wa magari kwenda Buguruni kwa wale wenye nia ya kuelekea Magomeni, Kinondoni, Oysterbay na Masaki,”ameeleza Diwani Klerruu.

Alisema kiasi cha sh.12,315,000,000 kimetumika katika sekta ya miundombinu na kwa ujumla kwa kipindi cha Mwaka 2020-2025.

Amewataka na kuwaonba wananchi wa Kata ya Mabibo, kuendelea kumuamini yeye, Rais Daktari Samia na CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2025 kwani kazi iliyofanyika ni kubwa na Mabibo inapiga hatua kubwa kwa Maendeleo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...