Na Diana Byera,Missenyi.


Wanafunzi na watoto ambao wako chini ya miaka 18 wilayani Missenyi mkoani Kagera,  wamehakikishiwa kuwa Siri zao wanazowasilisha katika madawati ya Polisi na Ustawi wa Jamii kuhusu ukatili unaowakumba shuleni na Majumbani zinalindwa hivyo wasiogope kutoa taarifa kwa vitisho wa Waharifu.

Timu ya Kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia "MSLAC" imekutana na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Minziro wilayani Missenyi yenye kidato Cha kwanza hadi cha sita ambapo Elimu ya kisheria kuhusu ukatili wa Kijinsia na njia za kufikia mamlaka husika katika kuhakikisha Changamoto zao zinasikilizwa na siri zinatunzwa na watuhumiwa kuchukuliwa Sheria.

Grace Matofali kutoka Dawati la Jinsia kitengo cha Polisi Missenyi ambaye pia ni miongoni mwa wataalamu wanaotoaa Elimu ya msaada wa kisheria,  licha ya kutoa Elimu kubwa juu ya madhara ya ukatili kwa jamii na changamoto zinazowakumba wanafunzi wa Sekondari,alisema Kuna wimbi la wahalifu wanaotoa vitisho kwa watoto wanaobakwa na kulawitiwa kuwa wakisema watauwa, jambo ambalo linatia hofu Watoto.

"Kwa upande wa Polisi tunapokea kesi 5 au 6 za maswala ya ubakaji na ulawiti na kesi nyingine za vipigo ni nyingi sana zaidi ya hata 50 kwa mwezi ,lakini Kuna kundi la wahalifu linalotisha watoto ,anambaka mtoto alafu anamwambia ukisema nitakuua,nitakunyonga,naomba niwahakikishie kuwa serikali imeweka ulinzi mkubwa kwa mtoto hivyo niwaondoe hofu njoo muwataje waharifu ,njoo mseme bila kuogopa tutawalinda kwa nguvu zote na kupambana na waharifu"alisema Matofali.

Hakika Ibrahim afisa ustawi wa jamii wilaya ya Missenyi alisema kuwa wilaya hiyo inapokea kati ya kesi 50 Hadi 60 kwa mwezi juu ya maswala mchanganyiko ya ukatili kuhusu watoto na malalamiko mengi yakiwa ni utekelezaji wa watoto ,mimba, ubakaji na ulawiti jambo ambalo ni changamoto kwa watoto walioko chini ya miaka 18

Alisema kwa sasa Serikali imeweka mkazo sana na kushughulikia wahalifu ambao wamekuwa wakitenda matukio ya ukatili kwa watoto wakiwemo wanafunzi ambapo hivi karibuni Kuna baba wa mtoto amehukumiwa miaka 30 kwa kumpa mtoto wake mimba na akadai kuwa serikali ya wilaya ya Missenyi imefanikiwa kumrejesha mwanafunzi mmoja na kumpeleka kidato cha kwanza baada ya wazazi wake kumtorosha ili kumpeleka katika wilaya ya Rongido kufanya kazi hivyo watoto wasigope kutoa taarifa.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...