NA WILLIUM PAUL, HAI.

MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewataka wananchi mkoani humu kuendelea kuuenzi, kuudumisha na kuulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kutowapa nafasi baadhi ya watu wenye chokochoko ya kutaka kutia maneno ya chuki kuhusu Muungano.

Babu alitoa kauli hiyo leo alipokuwa akiwahutubia Wananchi wa kijiji cha Mkalama kata ya Rundugai wilayani Hai mkoani Kilimanjaro ambapo maadhimisho hayo yalifanyika kimkoa kwa kupanda miti 15000 katika eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na badae kuzungumza na wananchi.

Alisema kuwa, muungano huo umepelekea Wananchi kutoka Tanzania bara kwenda Zanzibar kifua mbele huku wengine wakitoka Zanzabar kuja Tanzania bara kifua mbele ambalo yote hayo yamechangiwa na uwepo wa muungano huo.

“Watanzania bara wengi wapo Zanzibar wanapata elimu na wapo Wazanzibar wanapata elimu kwenye vyuo vikuu na vyuo vingine kwa uhuru na upendo mkubwa kwa sababu ya tunu ya muungano wetu hivyo Wanakilimanjaro tunawajibu wa kuendelea kuulinda muungano” alisema Babu.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa, viongozi wameweza kuwaweka wananchi pamoja na kuhakikisha dosari za muungano zilizokuwa zinasemwa zimetatuliwa ambapo kwa sasa zimebaki tatu ambapo nazo zinafanyiwa kazi.

Alisena kuwa, Watanzania wanayo kazi ya kuendelea kuulinda Muungano na kutowapata nafasi baadhi ya watu wenye chokochoko za kutaka kutia maneno yao ya chuki kuhusu muungano na kuwataka kuulinda kwa nguvu zao zao.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...