Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaendelea na utekelezaji wa mradi wa kupeleka umeme katika migodi midogo ya Bagamoyo, ikiwemo maeneo ya wazalishaji wa chunvi mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi DM Company Limited.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, leo Aprili 8, 2025, wakati akijibu swali la Mbunge wa Bagamoyo, Muharami Shabani Mkenge, bungeni Jijini Dodoma, Mbunge Mkenge alihitaji kujua ni lini umeme utapelekwa katika eneo la Kitame, Kata ya Makurunge, ili kusaidia wazalishaji wa chunvi.
Kapinga alieleza kuwa hadi kufikia mwezi Machi mwaka 2025, jumla ya maeneo 14 ya migodi tayari yalikuwa yamepatiwa umeme, ikiwemo migodi mitatu ya chunvi katika eneo la Kitame, Kata ya Makurunge, Aliendelea kusema kuwa jumla ya wachimbaji 34 tayari wamepatiwa huduma ya umeme.
Mbunge wa Kibiti Twaha Mpembenwe, alitoa pongezi na shukrani kwa serikali kwa juhudi zinazofanywa katika kupeleka umeme katika jimbo lake, huku akiiomba serikali kuhakikisha maeneo mengine ya vitongoji ambayo bado hayajafikiwa na huduma hiyo yanapata umeme.
Akitoa maelezo zaidi kuhusu ombi hilo, Naibu Waziri Kapinga alisema kuwa serikali itaendelea kupeleka umeme katika maeneo ya vitongoji, ikiwemo Kitame, na kwamba wananchi wa eneo hilo watanufaika zaidi kutokana na utekelezaji wa mradi huo. Alisisitiza kuwa utekelezaji wa miradi ya umeme unategemea upatikanaji wa fedha, na kwamba serikali itaendelea kufanya juhudi kuhakikisha kuwa huduma hii inawafikia wananchi wote.
Kapinga pia alifafanua kuwa miradi inayotekelezwa nchini inasimamiwa vyema na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dotto Biteko, na kwamba juhudi za serikali na usimamizi mzuri wa sekta hiyo umesaidia kufanikisha utekelezaji wa miradi hiyo kwa ufanisi.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kapinga alimhakikishia Mbunge wa Kilombero kuwa mkandarasi wa utekelezaji wa mradi wa kupeleka umeme kwenye vitongoji 15 vya jimbo lake ameshapatikana na tayari ameshaanza kazi katika Mkoa wa Morogoro. Alisema kuwa Wizara ya Nishati itahakikisha mkandarasi huyo anapata usimamizi wa kutosha ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa haraka na kuanza kufikia wananchi wa jimbo hilo.
Utekelezaji wa miradi ya umeme ni sehemu ya juhudi za serikali za kuboresha huduma za nishati katika maeneo mbalimbali ya nchi, hususan maeneo ya vijijini na migodi midogo, ili kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...