SERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo ilitangaza tarehe 23 Aprili 2025, kuzuia mazao kutoka nchi za Afrika Kusini na Malawi kuingia katika mipaka ya Tanzania hadi hapo hatua zitakapochukuliwa kwa nchi hizo kuruhusu mazao yetu kuingia katika masoko yao.

Kufuatia zuio hilo, Serikali za Malawi na Afrika Kusini zimewasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Kilimo za Tanzania ili kuweza kutafuta suluhisho la zuio husika.

Taarifa kwa umma iliyotolewa na Waziri wa Kilimo Hissein Bashe imeeleza kuwa makubaliano yaliyofikiwa ni kwamba Serikali ya Malawi itatuma ujumbe wake tarehe 2 Mei 2025 utakaoongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje akiambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara na Waziri wa Kilimo ili kukutana na jumbe wa Tanzania jijini Dodoma chini ya uratibu wa Waziri wetu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kuhusu zuio la Afrika Kusini, majadiliano ya wataalam wa Wizara ya Kilimo kupitia Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania yanaendelea kwa pamoja na Mamlaka za nchi ya Afrika Kusini zinazohusiana na Afya ya Mimea na Masoko.

Kwa misingi hiyo, Wizara ya Kilimo inaondoa mazuio yote yaliyowekwa kwa nchi za Malawi na Afrika Kusini kuanzia tarehe 26 Aprili, 2025 tukiamini kuwa majadiliano yanayoendelea yataleta suluhisho.

Serikali inawahakikishia wakulima na wananchi wa Tanzania kwa ujumla kuwa, uhuru wa biashara ya mazao ya kilimo kulingana na mataka ya afya ya mimea, rasilimali za nchi zilizopo na mahusiano mapana ya kidiplomasia kwa faida ya wote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...