SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson amefungua Kongamano la Uhuru wa Wana Taaluma Afrika linalofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo wanataaluma zaidi ya 24 kutoka nchi mbalumbaliu barani Afrika wameshiriki.
Kongamano hilo limeanza leo Aprili 29 hadi Mei 2, 2025 limeandaliwa na Ndaki ya Sayansi za Jamii UDSM kwa ushirikiano na Kanseli ya Maendeleo ya Utafiti katika Sayansi za Jamii (CODESRIA).
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo, leo Aprili 29, 2025 Jijini Dar Es Salaam, Spika wa Bunge Tulia amesema kuwa wanataaluma hao watapata nafasi ya kujadili uhuru wa kusema mawazo yao kwa sababu wao ni watu wa utafiti, kujaribu kusema ule utafiti walioufanya na mambo ambayo wanatarajia kufanya kwenye jamii.
Amesema," Lazima wanataaluma kila mmoja kwenye taaluma yake, mawazo wanayoyafikiria watuletee ili kwenye jamii yetu tuweze kusonga mbele, tuweze kupiga hatua,".
" Zile changamoto walizosemawanataaluma hawa, mojawapo ni kuangalia namna ya wanavyoweza kuingiliwa na wanasiasa lakini viongozi wa kiserikali, Uhuru wa wanataaluma usiwe unaingiliwa na serikali, wana siasa hata wao kwa wao wameweza kufanya kazi kwa uhuru. Hata wao sasa hivi wanakiri umevuka mipaka ya kujadili na kusema," amesema.
Kwa upande wake Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii UDSM, Prof. Christine Noe amesema Mkutano huo wanarejea makubaliano waliyokubaliana kwa kuwa wanaona taaluma na wanataaluma sauti zao zimepotea na jamii inaona kuna umbwe wanataaluma hawapo tena.
Prof. Noe amesema, " Jamii haisikii matukio makubwa yanayoendelea, taaluma na wana taaluma hawasemi kwa sauti zinazosikika wakati huo tunafanya tafiti sana, tunaandika machapisho mengi lakini jamii inakosa ile taaluma,
"Viongozi nao wanakosa kujua kile tunachokifanya , tunajitathmini kazi yetu inakuja, sauti zetu hazisikiki, matokeo ya kazi yetu hayaendi mbali," amesema.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...