Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao nchini imetangaza kushiriki maandalizi ya Mtoko wa Pasaka utakaofanyika Aprili 20,2025 katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, ikilenga kuwaunganisha Watanzania kupitia nyimbo, maombi, na kutoa misaada kwa kina mama wajawazito
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam , Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Steven Mengele almaarufu Steve Nyerere, amesema kuwa tukio hilo litakuwa maalum kwa ajili ya kuliombea Taifa na pia kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan katika mwaka huu wa uchaguzi,pia Taasisi itatoa msaada kwa kina mama wajawazito katika hospitali zote za wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam kuelekea kilele cha Pasaka.
"Amani tuliyopewa na Mungu lazima tuilinde kwa gharama yoyote, Maombi yana nguvu kuliko mtutu wa bunduki, akina mama sasa hivi ndio wanaobeba taifa, Hii fursa ya kuwasaidia ni sehemu ya kazi yetu kama taasisi yenye lengo la kuongelea na kugusa maisha ya Watanzania kwa vitendo",amefafanua
Steve
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...