Na Issa Mwadangala.

Wafanyakazi wa Kampuni ya madini ya Makaa ya Mawe WAADHUHA (EA) TRADING COMPANY LIMITED iliyopo Kata ya Magamba Wilaya ya Songwe wametakiwa kujali usalama wao pindi wawapo kazini ili kujiepusha na majanga yanayoweza kuepukika.

Kauli hiyo imetolewa Aprili 25, 2025 na Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga wakati alipotembelea mgodi huo na kuongea na viongozi waandamizi ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa mgodini hapo kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu uchimbaji salama ikiwa ni muendelezo wa dhana ya ushirikishwaji wa jamii kwa makundi yote ili jamii iwe na uelewa kuhusu mambo mbalimbali ya usalama.

"Unapokuwa kazini au eneo la mgodi unatakiwa kuvaa mavazi rasmi ili kujikinga na majanga pindi yatokeapo hii itasaidia kuwaweka salama katika shughuli zenu za kila siku hapa mgodini" alisema Kamanda Senga.

Pamoja na elimu hiyo Kamanda Senga alitoa wito kwa wafanyakazi wa mgodini hapo kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe ili kuendelea kudhibiti matukio ya uhalifu na wahalifu katika maeneo yao.

Naye, Meneja wa Mgodi huo, Bi. Salome Nkurlu amesema wataendelea kulisimamia suala la usalama kazini kwani katika majukumu yao hakuna kazi bora dhidi ya usalama, aliongeza kwa kusema kuwa wataendelea kusimamia kanuni zote za usalama ili mali na wafanyakazi waendelee kufanya kazi katika mazingira salama ambayo hayataweza kuwasababishia madhara yoyote katika majukumu yao pindi wawapo kazini.

Kwa upande wake, Katibu wa Kampuni hiyo Bw. Enosy Kilufi amelishukuru Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe na kuahidi kuendelea kushirikiana nalo hasa katika masuala ya kiusalama kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kiujumla.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...