Na Diana Byera Bukoba,


Wakala wa Barabara TANROAD mkoani Kagera wamejipanga kukabiliana na athari za mvua ili kuhakikisha wanarejesha hali ya usalama wa Barabara mkoani Kagera kwa saa 24

Meneja wa TANROAD mkoani Kagera Ntuli Mwaikosesya amesema kuwa kutokana na Mvua kubwa iliyoanza kunyesha kuanzia Machi mwaka huu na zinazoendelea tayari timu ya wataalam wa uhandishi kutoka Ofisi yake wamejipanga na kukabiliana na athari zote za mvua inayoendelea kunyesha.

Amesema kuwa madhara yaliyotokea kutokana na mvua zilizoanza kunyesha Machi mwaka huu ni kwenye Barabara ya Kasozibakaya _Kabindi_Nyantakara yenye kilometa 82 ambayo imeharibika Sehemu kidogo na madhara yake yamekabiliwa ndani ya masaa 24 na sasa inapitika vizuri na wananchi wanapata huduma.

"TANROAD tunahudumia mtandao wa Barabara zenye kilometa 2072 , na sasa Barabara zote zinapitika vizuri kwa sababu tuna vifaa,mitambo, waandisi na wakandarasi wako tayari kwa dharura yeyote Ile ambayo itatokea wakati wa mvua , hii ni kuhakikisha wananchi hawakwami katika kupata huduma zote zinazohitajika ukizingatia kuwa tunaungana na nchi za Africa Mashariki hivyo tuko tayari kukabiliana na madhara ya Mvua"amesema Mwaikosesya

Amesema athari za mvua ya Elnino zilizosababisha madhara ya Barabara na uhalibifu mkubwa kwa Barabara maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera tayari matengenezo yake yamekamilika kwa gharama ya shilingi Bilioni 4.6

"Barabara ya Nyabihanga -Minziro,mtukula _Bukoba,Bugene_Kaisho, Rutenge kishoju zimekamilika kwa asilimia 100 na wananchi wanaendelea kupata Huduma kupitia Barabara hizo "amesema

Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari pale wakiona maji yakikatiza kwa Kasi katika Barabara madaraja,kupungusha Shughuli za kilimo karibu na Kingo za Barabara,kuacha Kuiba Alama za Barabarani , kuacha kutupa uchufu chini ya makatavati kwani hali hiyo imasababisha mitaro kuziba na kushindwa kupitisha maji .

TANROAD mkoa wa Kagera imetenga bajeti ya Bilioni 12 kwa mwaka 2024/2025 kwa ajili ya matengenezo ya kawaida ya Barabara hali inayopelelea kukabiliana na dharura wakati wowote.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...