Mhadhiri, Mwandishi wa vitabu na Mchoraji Maarufu  wa Chuo Kikuu cha Sultan Quaboos  cha nchini Oman, Prof. Ibrahim Noor ameishukuru serikali kuendelea na jitihada za  kuitangaza Lugha ya Kiswahili duniani kote na kuwaomba watanzania wote nchini  kuendelea kukuza lugha ya Kiswahili ili iendelee kuzungumzwa na watu wengi duniani kote.

Ameyasema hayo leo tarehe 12/04/2025 wakati akiwasili   nchini kutokea Mascut kupitia Zanzibar amesema kuwa ni lugha yenye kupendwa na kuzungumzwa na wengi sasa duniani kote na kuwaomba watanzania wote duniani kuendelea kutangaza Lugha ya Kiswahili.

“Lugha hii imekuwa kubwa na kupendwa na watu wengi nchini, hivyo nawaomba wote duniani tuendelee kuunga mkono juhudi za watu waliotangulia kukitangaza Kiswahili  na wengine waendelee zaidi” amesema Prof. Noor. 

Vilevile,  ameipongeza  serikali kwa kuanzisha tuzo  kwa waandishi bunifu ni kuthamini  jitihada za kukuza kiswahili na kuchochea usomaji nchini.

 Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba aliongoza mapokezi ya Prof. Noor akiwa sambamba na  Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo, Prof. Penina Mlama na watumishi wengine wa  TET. 

Prof. Noor ni mgeni maalumu atakayeshiriki hafla ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu itakayofanyika kesho tarehe 13/04/2025 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango.

Tuzo hizo zitafanyika kwa mara ya tatu mfululizo ambapo, washindi watakabidhiwa zawadi za pesa taslimu pamoja na vyeti.

Tuzo hizo zitafanyika kwa mara ya tatu mfululizo ambapo, washindi watakabidhiwa zawadi za pesa taslimu pamoja na vyeti.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...