Na Diana Byera,Bukob.

Waziri wa Katiba na Sheria   Dkt.Damas Ndumbalo amewataka Watanzania Kupuuza maneno ya Wanasiasa wanaopita maeneo mbalimbali   nchini na kueneza habari za uchochezi kuhusu maswala ya Uchaguzi mkuu na kudai kuwa siasa hizo zinavunja Katiba ya Nchi.

Waziri Dkt. Ndubaro amesema kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka bayana sababu zinazoweza kusababisha Mtanzania kutoshiriki uchaguzi na imebainisha uchaguzi kama haki ya Msingi ya Kila mwananchi mwenye umri wa kuanzia miaka 18  na kuendelea, hivyo kumzuia kushiriki ni kumnyima haki yake ya kibinadamu.

Waziri Huyo wa Katiba na Sheria Dkt. Ndumbaro aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kampeini ya kisheria katika mkoa wa Kagera iliyofanyika katika viwanja vya Mayunga vilivyopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, ambapo  mamia ya wananchi  wamejitokeza  kuleta changamoto   zao za kisheria na kuziwasilisha kwa wanasheria huku wengine wakipata Fursa ya kukabidhiwa mawakili mbele ya Waziri huyo.

Kupitia Kampeini hiyo amewahakikishia wakazi wa mkoa wa Kagera kuwa kampeini hiyo ni endelevu na tayari wizara imewaajili maafisa Dawati wa kushughulikia  malalamiko ya kisheria wilayani wapatao 400 nchi nzima, huku wanasheria  wasaidiz waliopewa  mafunzo  kwa ajili ya kutoa huduma za kisheria wamefikia 2,500.

"Wananchi msiwe na wasiwasi tumeshuhudia mafanikio makubwa sana kupitia kampeini ya mama Samia ya msaada wa kisheria na toka kampeni hii ianzishwe mwaka 2023 Asasi za kiraia zinazotoa  huduma za kisheria zimeongezeka  kutoka 85 Hadi 387"alisema Ndumbalo.

Alitoa wito kwa viongozi wa Dini kutoacha kukemea wananchi wanaojichukulia Sheria mkononi, kwani wanageuka chanzo cha mitafaruku na migogoro iisiyoisha ,pia amezitaka familia kutafuta suluhisho la kupatana kwani familia nyingi ndizo chimbuko la migogoro ya Ardhi na Miradhi.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa alisema kuwa, mkoa huo utawavua mamlaka Wenyeviti wa vijiji na Mitaa pamoja na kuwatengua  watendaji wa mitaa na vijiji wanaosababisha migogoro ya Ardhi kwani wao wamekuwa chanzo cha  migogoro ya Ardhi mara kwa mara

"Mkoa wa Kagera huu hata vitendo vya mauaji mara nyingi vinasababishwa na migogoro ya Ardhi ,mara nyingi  wenyeviti wa  vijiji wanauza maeneo ya wananchi migogoro haiishi na  hapohapo tunapata watu wanalipiza visasi ,sasa kama mkoa tunapanga kuchukua hatua madhubuti ,kuwawajibisha"alisema Mwassa 

Aidha ameipongeza Mahakama kuu Kanda ya Bukoba na Mahakama ya Hakimu mfawithi wilaya ya Bukoba kwa jinsi wanavyoendelea  kupambana na  kesi za ukatili wa Kijinsia  na kuhakikisha kuwa watuhumiwa wa vitendo vya ubakaji na ulawiti wanavyowajibishwa kisheria .



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...