Na Diana Byera,Missenyi

Baadhi ya Wazee wilayani Missenyi wamepongeza Kampeni 
ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia na kueleza kuwa imeleta mwanga mkubwa katika utatuzi wa changamoto za ufahamu kuhusu masuala ya umiliki wa Aridhi,Kuandika Wosia pamoja kuandaa wasimamizi wa Mirathi.

Kampeni ya Msaada wa Kisheria wilayani Missenyi imeingia siku ya tatu ikiwa inaangazia Utatuzi wa migogoro ya kisheria, usaidizi wa Kisheria pamoja na utoaji wa Elimu ya kisheria katika Nyanja za Mirathi,Wosia,ukatili,Ardhi,malezi, ajira madai,huku Wazee wilaya ya Missenyi katika vijiji mbalimbali wakipongeza hatua ya serikali ya kuwafanya wananchi kuwaelimisha pamoja na kutatua changamotoo zao.

Alexander Kayombo mkazi wa Kijiji Cha Bubale kata Kakunyu wilayani Missenyi alisema kuwa moja ya changamoto kubwa kwa sasa kwa wazee ni ukatili na Unyanga'nyi juu ya masuala ya Ardhi pamoja na ukosefu wa Elimu hasa kwa vijana wadogo ambao wanaongoza kwa kuvunja Sheria.

"Nina miaka 78 ,sijawahi kufuatwa na Wakili au mwanasheria kuja kijijini kutusikiliza ,kwa mara ya kwanza nimeona serikali imetuma mawakili wa Kijiji Cha mpakani kuja kutoa Elimu na kupokea changamoto za kisheria bila kwenda kusimama kizimbani , hii ni hatua kubwa sana kwetu ,pamoja na miradi mikubwa tunayoona lakini hili ni suala la kugusa hisia za mtu moja kwa moja na ni Faraja"

Leonia Aloyce Miaka 90 mkazi wa Missenyi ameguswa moja kwa moja na Elimu ya usimamizi wa Mirathi kisheria na kudai kuwa haijawai kutokea wananchi wanakapata Elimu ya usimamizi wa Mirathi adharani na wengi wanadhani kuwa familia zenye wasimamizi wa Mirathi ni familia zenye uwezo kumbe hata watu wa kawaida wanaweza kuandaa wasimamizi wao.

Aidha wananchi wa Kijiji Cha Bubare wamepongeza hatua za Halmashauri ya wilaya ya Missenyi kuangazia Kijiji Chao na kuwahaidi wananchi kuwa Kijiji icho Kiko kwenye mipango ya kuwapatia hati wananchi wake kwa sababu ni moja ya Kijiji kinachokua.

Akitoa Elimu ya Kisheria juu ya maswala ya Ardhi kupitia kampeini ya msaada wa kisheria ya mama Samia afisa mipango miji na vijiji wilayani Missenyi Deliqueen Lyimo alisema kuwa Kijiji icho kimeonekana kuwa kinakua kwa Kasi hivyo halmashauri Iko tayari kuanza kutoa hati miliki za viwanja kwa mujibu Sheria no 4 ya Ardhi ya mwaka 1994 na wengine ambao maeneo yao hayajakua watapata hati za kimila kwa mujibu wa Sheria no 5 ya Ardhi ya mwaka 1999

"Tayari tumepima Kijiji chenu na tumeona kinakua kwa Kasi ndio maana leo kupitia kampeini ya msaada wa kisheria ya mama Samia tunatoa Elimu za umiliki wa Ardhi na maswala ya hati ili muelewe kuwa mama amedhamilia kuwaokoa wananchi wenu na watoto wenu kwa sababu Ardhi ikishamilikiwa haifutwi na mtu unaweza kutumia Ardhi Yako kufanya biashara,kukopa ,na kufanya uwekezaji"alisema Lyimo

Hatua hiyo na Elimu juu ya masuala ya Hati imefurahisha vijana wazee na wananchi wa Bubale kwa ujumla na kudai kuwa hiyo ni habari njema na hawatachezea Fursa juu ya kumiliki maeneo yao kihalali.

Mratibu wa kampeini ya msaada wa kisheria ya mama Samia Wilayani Missenyi Maxmillan Fransis alisema kuwa ndani ya siku 3 mfululizo maswala yaliyojitokeza katika wilaya hiyo yanayohitaji utatuzi wa Haraka ni Mirathi pamoja na changamoto za Ardhi na kudai kuwa Mpaka sasa Kupitia kampeini hiyo amewasiliana na mamulaka na wanasheria ili kuhakikisha kampein hiyo haiachi Dukuduku kwa mwananchi na utatuzi unapatikana.

"Tayari tunasiku 3 mamia ya wananchi wanajitokeza kupata Elimu ya msaada wa kisheria na wengine wanachangamoto zao mpaka sasa changamotoo za Mirathi na Ardhi ndizo zinazoongoza kuletwa na wananchi tunapokea zote na tunazipati ufumbuzi hatutaacha migogoro kupitia kampeini ya Mama Samia Kila changamotoo itatatuliwa na changamoto kubwa inayoendelea mahakamani kama mwananchi Hana Wakili tunampatia Wakili ili haki itendeke".





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...