Dar es Salaam, Mei 15, 2025.
KWA kuendeleza mkakati wake wa kukuza upatikanaji wa huduma bora na za haraka kwa wateja, Airtel Tanzania imezindua rasmi maduka mapya manne ya huduma kwa wateja katika maeneo ya Sinza, Mikocheni, Mwananyamala na Magomeni, jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huu ni sehemu ya mpango wa kimkakati wa Airtel wa kuimarisha uwepo wake wa kimataifa kwa njia ya ukaribu wa ndani, ukilenga kuwafikia wateja milioni 20 nchini kwa huduma zinazokidhi mahitaji ya kidijitali kwa sasa.


Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika duka la Sinza, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Adrianna Lyamba, amesema;

"Kupitia mkakati huu, Airtel inahakikisha kuwa huduma za msingi kama Airtel Money, usajili wa laini, mauzo ya vifaa na huduma zingine za kiufundi zinapatikana kwa urahisi zaidi, kwa wakati, na kwa ubora wa hali ya juu. Tunaboresha uzoefu wa mteja kwa kuhakikisha huduma zinamfikia popote alipo."

Maduka haya yameanzishwa baada ya utafiti wa mahitaji na mrejesho wa wateja, ikiwa ni hatua mahsusi ya mkakati wa Airtel wa kujenga urahisi wa upatikanaji wa huduma, kukuza ujumuishwaji wa kidijitali, na kupunguza hatari za usalama wa taarifa kwa kuwa na vituo rasmi vya msaada.

Kupitia huduma zinazotolewa ikiwemo usaidizi wa usalama wa taarifa dhidi ya utapeli wa mtandaoni sambamba na kampeni ya serikali ya #Sitapeliki—maduka haya yamejikita katika kuimarisha uhusiano salama kati ya wateja na huduma za kidijitali.

"Tunaamini kila duka lina nafasi ya kuwa kituo cha mabadiliko—si tu kwa kutoa huduma, bali kwa kuwa jukwaa la kujifunza, kufikia teknolojia mpya na kujenga uchumi wa kidijitali," ameongeza Lyamba.

Kwa muundo wa kisasa unaochanganya teknolojia na ubunifu wa huduma, maduka haya ni sehemu ya mkakati mpana wa Airtel wa kuleta uvumbuzi, upatikanaji na unafuu kwa kila mteja.

Amesema kuwa uzinduzi huo ni moja ya upanuzi wa Mtandao wa Huduma katika  Kuongeza vituo vya kimkakati vya utoaji huduma.

Kupunguza umbali kwa mteja kufuata huduma, Uimarishaji wa Usalama: Kutoa msaada dhidi ya utapeli wa mtandaoni.

Kukuza Ujumuishwaji wa Kidijitali ili kuwasaidia Watanzania kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali.

Kuboresha Uzoefu wa Mteja kwa Huduma bora, haraka, na zinazojibu mahitaji ya wakati.

Hatua hii inaweka Airtel Tanzania kwenye mstari wa mbele kama mtoa huduma anayelenga mteja kwanza kwa kutumia mkakati wa kisasa, jumuishi na unaoendeshwa na teknolojia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...