Na Mwandishi wetu
Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya Metrolife imezindua ya Kampeni ya Bima ya Vikundi Kidijitali iliyozinduliwa na Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania -TIRA Dkt Baghayo Saqware.
Uzinduzi huo umefanyika Jijini Dar es salaam Mei 29 ,2025 huku Dkt Saqware akiipongeza NMB kwa ubunifu wa Uwekezaji katika Teknolojia ya kisasa katika kutafuta masuluhishi ya changamoto mbalimbali hasa ya Bima ya Vikundi.
Aidha Dkt Saqware alisema Benki ya NMB ni Benki ambayo imekuwa ikiunga mkono ajenda ya Serikali ya kuhakikisha watanzania wengi wanakata Bima ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza utegemezi katika jamii.
Alisema ushirikiano kati ya Benki ya NMB na Kampuni ya Bima ya MetroLife utasaidia watanzania wengi kupata elimu ya Bima na kukata Bima kwa manufaa yao na jamii.
“NMB nawashukuru sana mmekuwa wabunifu kusukuma ajenda ya Serikali katika kuhakikisha watanzania wengi wanatumia huduma za bima”Alisema Dkt. Saqware
Alisema uzunduzi wa Bima ya Vukundi inakwenda kuwa mkombozi wa wananchi wengi ambao wapo katika vikundi kwa kuwa wengi wa wananchi wanamiliki simu ambazo ni rahisi kujiunga na Bima.
Amewataka Benki ya NMB kuhakikisha wanaendelea kusukuma ajenda ya ukataji Bima kwa watanzania kwa kuwa bado idadi ya waliokata bima ni ndogo na kusababisha kuwepo kwa utegemezi mkubwa.
Kwa upande wake Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi alisema Bima ya Vikundi inakwenda kuwakombozi wa watanzania wengi watakaokuwa katika vikundi ambavyo watachangia fedha kidogo kwa kila mmoja kuanzia shilingi Mia Tano ambayo itamfaidisha mwanachama atakayepata misiba itakayompa mkono wa pole hadi Shilingi Milioni Moja.
Amewataka watanzania kuchangamikoa fursa iliyoletwa na Benki ya NMB na Bima ya Metro-Life ya Mkono wa pole kwa vikundi huku akisema huduma hiyo huduma hiyo tayari imeanza.
“Sasa leo hii bima ya mkono wa pole ambayo tunafanya sisi na mdau wetu MetroLife tumeingiza na yenyewe kwenye jirani,kwa hiyo NMB jirani anaweza kukupatia Bima ya Kikundi”alisema Mponzi
Mponzi amewataka watanzania kuhakikisha wanafungua akaunti na Benki NMB kwa kuwa imekuwa ikitoa masuluhishi mbalimbali bila kufika katika matawi yaliopo nchi nzima.
Mapema katika katika mdahalo Mkuu wa Idara ya Bima wa Benki ya NMB Martine Massawe alisema kwa sasa wameitoa Bima katika matawi na kuifikisha mkononi ili kupeleka huduma hiyo karibu na wananchi.
Massawe alisema kwa sasa wameboresha huduma hiyo ya Bima kwa kutoa malipo chini ya Saa 48 ili kuondoa usumbufu kwa wateja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...