Na Diana Byera Bukoba,
Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini chama Cha Mapinduzi CCM Jason Rweikiza Ameishukuru serikali kwa kuleta fedha za miradi ya maendeleo shilingi Bilioni 126.6 na kudai kuwa wananchi wa Jimbo hilo hawadanganyiki kwa kauli za kuwaadaa badala yake watamchagua Dkt Samia Kwa ajili ya maendeleo zaidi.
Akitoa salamu kwa maelfu ya wakazi wa mkoa wa Kagera waliojitokeza kupokea na kumsikiliza Katibu wa itikadi Siasa na uenezi Amos Makala Rweikiza amesema kuwa katika Jimbo la Bukoba Vijijini Kuna maendeleo makubwa sana na miradi inayogusa wananchi wengi Wa hali za chini inayoendelea kutekelezwa na serikali.
"Hatuwezi kudanganyika ,kwa sasa vijiji vyote Vina umeme na serikali inaendelea kusambaza katika vitongoji,Vituo vipya vya afya,Elimu madarasa yameota kama uyoga, Upatikanaji wa huduma ya maji, kilichobaki mwezi Octoba ni kukichagua chama Cha Mapinduzi Kwa mara nyingine na CCM kupata ushindi wa kishindo"Amesema Rweikiza
Aidha Ameishukuru serikali kwa kuanza utekelezaji wa miradi wa ujenzi wa madaraja makubwa ya Kyenyabasa na kalebe ambayo kwa miaka Mingi ni kero kwa Wanachi hasa nyakati za mvua ambapo amedai kuwa madaraja hayo yakikamilia wananchi watapunguza adha hasa katika swala la kusafiri
Alisema anashuhudia Kasi ya utekelezaji wa Miradi mikubwa ambayo ilishindikana kwa miaka Mingi ambapo amewaomba wananchi wa Jimbo Hilo kuendelea kukiamini chama Cha Mapinduzi Kwa ajili ya maendeleo yao ya sasa na vizazi vijavyo.
Katibu wa Itikadi ,siasa na uenezi Amosi Makala amemuhakikishia Mbunge huyo kuwa miradi ambayo wakandarasi wake wako kazini na ambao miradi imetekelezwa na hawajalipwa atawasiliana na waziri wa ujenzi na waziri wa fedha ili wakandarasi hao walipwe haraka iwezekanavyo.
Amewataka wakazi wa mkoa wa Kagera kutunza amani na kutojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa Amani kwani wavurugaji wa siasa waliowengi tayari wametafuta makazi mbadala kwa ajili ya familia zao wakati watanzania wengine wakiwa hawana sehemu nyingine ya kukimbilia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...