Mkufunzi wa Chuo cha Afya Excellent Rogers Gidion akitoa maelezo kuhusiana na kambi walivyoendesha katika utoaji wa uchunguzi na matibabu kwa wakazi wa Kibaha.
Mkurugenzi  wa Vyuo vya Afya na Sayansi Shirikishi vya Excellent, Msaada Balula akizungumza wakati wa kilele cha kambi ya uchunguzi na magonjwa mbalimbali iliyoendeshwa na Chuo hicho Kibaha mkoani Pwani.



Matukio mbalimbali katika picha wakati utoaji wa huduma ya uchunguzi na matibabu bure yaliyoendeshwa na Chuo cha Afya cha Excellent .
Mkazi wa Kibaha Fatuma Ng'itu akizungumza kuhusiana  na huduma aliyoipata katika kambi ya uchunguzi na matibabu bure iliyoendeshwa na Chuo cha Afya cha Excellent.
Mwanafunzi wa cha Afya cha Excellent Genelyce Ishuza akitoa elimu kuhusiana na ugonjwa wa kisukari katika Kambi ya Uchunguzi na Mabatibu bure iliyoendeshwa na chuo hicho.

*Ni katika kambi walionzisha katika kufanya uchunguzi na matiabu kwa kipindi cha mwezi mmoja bila malipo


Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

CHUO cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Excellent Kibaha mkoani Pwani kimefunga kambi ya kutoa huduma za afya kwa wananchi wa Mkoa ambapo wametoa huduma hiyo zaidi ya wananchi 500 huku wengine wakipata rufaa kutokana na uchunguzi waliofanya.

Chuo hicho kuendesha kambi hiyo ni kurudisha mchango kwa jamii inayozunguka katika kuangalia afya zao.

Akizungumza na waandishi wa habari wa Kambi hiyo Mkurugenzi wa Vyuo vya Afya na Sayansi Shirikishi vya Excellent, Msaada Balula amesema kuwa umekuwa ni utaratibu wa katika kutoa huduma hizo katika maeneo ya vyuo kutokana kunauhitaji wananchi kupata huduma za afya kwa kuanzia vipimo pamoja na kila mwananchi kutambua afya yake mara baada ya kufanya uchunguzi wameweza kuhudumiwa kupewa ushauri na wengine kuwapa rufaa.

Amesema kuwa kambi hiyi imeweza kutoa mwanga katika kutengeneza utaratibu wa mara kwa mara kwani uhitaji ni mkubwa.

Balula amesema kozi wanazozifundisha wanaonq vema kuanzia kwa wananchi wanaozunguka kuhudumiwa wanafunzi pamoja na madaktari ambao ni wakufunzi katika Chuo.

Balula amesema kuwa kuwa wananchi wanahitaji huduma za afya ikiwemo uchunguzi wa magojwa mbalimbali ambapo wakati mwingine wanakosa fedha ya kufanya uchunguzi hivyo kusogeza huduma hiyo kwa wale wanaokosa fedha kupata huduma kupitia kambi wameweza kupata bila kutumia gharama yeyote.

Amesema serikali ya awamu ya sita imefanya kazi ya kujenga kwa kujenga Hospitali,Vituo vya Afya ,Zahanati pamoja na Dispensari na kazi ya wadau imebaki kuwaanda rasilimali watu wa kwenda kuhudumia maeneo hayo.

Amesema Chuo cha Excellent kimeweka mikakati ya kuhakikisha rasilimali watu ya sekta inapatikana ya kutosha katika vyuo vyao.

Amesema kuwa katika vyuo vya excellent wamekuwa na utaratibu wa kuchangia damu ambapo ambapo wameweza kuchangia damu chupa 1000 ambapo na kibaha wanatarajia kuchangia damu chupa 200.

Mwananchi wa Kibaha Edinesta Paulo amesema wanashukuru Chuo cha Excellent kupeleka huduma za uchunguzi wa maginjwa mbalimbali kutokana na changamoto za uchumi wanashindwa kufanya uchunguzi afya zao.

Amesema kuwa kambi hiyo wanaomba kwa Chuo kuendelea kutoa mara kwa mara kwani msaada mkubwa kwao katika kujua afya kwani afya ndio msingi wa maendeleo.

Nae Fatuma Ng'itu amesema katika kambi hiyo wameweza kupata elimu ya magojwa yasio ya kuambukiza yakiwemo Sukari pamoja shinikizo la damu BP.

Amesema kuwa wakati mwingine wanapata magonjwa kutokana na kukosa elimu kujikinga nayo na kutaka kuwepo na mwendelezo wa kambi.

Jackson Gidion Mkazi wa Kibaha amesema kuwa Chuo Excellent kimekuwa muokozi kwa wakazi wa Mkoa wa Pwani katika utoaji wa huduma za matibabu na uchunguzi bure.

Mkufunzi wa Chuo cha Afya cha Excellent Dkt. Rogers Adrian amesema kuwa wananchi 500 wameweza kuhudumiwa katika Kambi ya utoaji wa matibabu na uchunguzi iliyoratibiwa na Chuo.

Amesema kuwa katika utoaji wa matibabu na uchunguzi wamekuwa na utaratubu wa kutoa elimu ya magonjwa mbalumbali na namna ya kujikinga nayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...