Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania, Fatma Kange kulia na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TBS, Kandida Shirima wakibadilishana mikataba mara baada ya kusaini makubaliano ya ushirikiano kati ya BRELA, GS1 pamoja na TBS. Mikataba hiyo imesainiwa leo Mei 20, 2025 jijini Dra es Salaam.

Mikataba ikioneshwa mara baada ya kusainiwa kwaajili ya makubaliano ya pamoja ili kukuza biashara nchini.

Picha ya pamoja ya baadhi ya wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa za ndani mara baada ya kupata Msimbomilia kwenye uzalishaji wa bidhaa za ndani.
Waziri wa Biashara, Dkt. Seleman Jafo akiwadkabidhi mfano wa Msimbomilia kwaajili ya bidhaa zao.
Waziri wa Biashara, Dkt. Seleman Jafo akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini mikataba ya makubaliano kati ya GS1, TBS, na BRELA.
Matukio mbalimbali.
Dar es Salaam, Mei 20, 2025
WAZIRI wa Viwanda, Dkt. Selemani Jafo amesema kuwa urasimishaji wa biashara ndogo na za kati (SMEs) kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) unaiwezesha Serikali kupata takwimu sahihi kuhusu biashara nchini, hatua inayosaidia katika kupanga sera madhubuti za kiuchumi.
Dkt. Jafo ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya BRELA, Shirika la Viwango Tanzania (TBS), na GS1 Tanzania, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa biashara rasmi huchangia kwa kiasi kikubwa mapato ya serikali kupitia kodi na ada mbalimbali, na kwamba ushirikiano huo utasaidia pia kupambana na bidhaa bandia na zisizo na viwango, ambazo zimekuwa changamoto kwa usalama wa walaji.
"Ushirikiano huu utarahisisha kwa kiasi kikubwa kazi ya watunga sera kwa kuwapatia taarifa sahihi kuhusu mazingira ya biashara, pamoja na bidhaa zinazozalishwa au kuuzwa nchini," alisema Dkt. Jafo.
Kwa upande wake, mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Bi Kandida Shirima, alisema kuwa TBS ina jukumu la kuthibitisha ubora wa bidhaa kwa kutoa alama ya ubora, ambayo huongeza uaminifu wa bidhaa hizo sokoni.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania, Bi Fatma Kange, ameeleza kuwa wamekuwa wakikutana na viwanda vidogo pamoja na wajasiriamali wadogo, na kuwapatia mafunzo kuhusu namna ya kufungua biashara zao na kutumia mfumo wa barcode katika kutangaza bidhaa zao kwa ufanisi.
“Msimbomilia (barcode) kutoka GS1 hutambulika kimataifa na hurahisisha biashara kuvuka mipaka ya nchi. Hii inawawezesha wafanyabiashara kuingia kwenye maduka makubwa na masoko ya nje kwa urahisi zaidi,” alisema Bi Kange.
Mkurugenzi Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa, amesema kuwa kupitia ushirikiano huu, mjasiriamali ataweza kusajili biashara kwa haraka na kidijitali, jambo litakalowarahisishia kuanza na kuendesha biashara zao kwa ufanisi.
Ameongeza kuwa bidhaa zilizosajiliwa rasmi na kuwa na barcode zitapata nafasi kubwa zaidi katika masoko makubwa na hivyo kuongeza ushindani wa biashara ndani na nje ya nchi.
Aidha, mfumo wa barcode kutoka GS1 unahakikisha uwazi na ufuatiliaji wa bidhaa, ambapo mteja anaweza kufahamu chanzo cha bidhaa anayonunua, na kuhakikisha kwamba inanunuliwa kutoka kwa chanzo halali.
Ushirikiano huu wa taasisi hizi tatu BRELA, TBS, na GS1 unahamasisha biashara rasmi, bidhaa bora, na uchumi shindani. Pia ni hatua muhimu inayoiwezesha Tanzania kujipanga vyema katika soko la kikanda na kimataifa.
Licha ya hayo GS1 Tanzania wamekata keki kusheherekea miaka 14 tangu kuanzishwa kwake na kugawa kwa kila muslikwa kufurahia siku hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...