Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi leo tarehe 10 Mei, 2025 amefanya ziara katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwepo mradi wa Ujenzi wa Jengo la kisasa la Makumbusho ya Jiolojia, Ujenzi wa Jengo la Makao makuu ya NCAA linalojengwa nje ya Hifadhi ya Ngorongoro katika Wilaya ya Karatu.
Ujenzi wa Miradi hiyo imefikia zaidi ya asilimia 90 na inatarajiwa kukamilika hivi Karibuni.
Dkt. Abbasi amesisitiza Menejimenti ya NCAA ikiongozwa na Kamishna wa Uhifadhi Dkt. Elirehema Doriye kuendelea kusimamia utekelezaji wa Miradi hiyo na kuhakikisha inakamilika kwa wakati, kuzingatia thamani ya fedha na viwango vya kimataifa kwa ajili ya kuhudumia wageni wanaotembelea hifadhi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...