Ecobank Tanzania imejivunia kushiriki na kuunga mkono Mkutano wa Mwaka wa Ushauri wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) kwa mwaka 2025 uliofanyika tarehe 15 na 16 Mei 2025 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Mgeni rasmi wa mkutano huo alikuwa Waziri wa Ujenzi Mh. Abdallah Ulega (Mbunge).

CRB ilianzishwa chini ya Sheria ya Usajili wa Makandarasi, Sura ya 235 (Rejeo la 2002), ikiwa na dhamira ya kudhibiti na kuendeleza sekta ya ujenzi ili kuwa ya ushindani na endelevu, kwa kuwa na wakandarasi wenye uwezo wa kutoa kazi zenye ubora na kuzingatia usalama, kwa lengo la kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

Ecobank ilishiriki katika mkutano huu muhimu kama sehemu ya dhamira yake ya kusaidia ukuaji na mageuzi ya sekta ya ujenzi na miundombinu nchini. Ikiwa na uwepo katika zaidi ya nchi 33 barani Afrika, Ecobank ina uzoefu mkubwa katika kusaidia miradi mikubwa ya miundombinu pamoja na biashara ndogo na za kati (SMEs) kupitia bidhaa za kidijitali za kibenki, suluhisho za fedha za biashara (trade finance), na programu za kukuza uwezo wa wajasiriamali.

Akizungumza kwenye mkutano huo Mkuu wa Kitengo cha Biashara kwa Wateja Wakubwa (Commercial Banking) Joyce Ndyetabura alisema wanatambua mchango mkubwa wa wakandarasi katika kuleta maendeleo ya kitaifa hivyo mkutano huo umewapa fursa nzuri ya kuwafikia wakandarasi na kuwapatia suluhisho sahihi kwa biashara zao,.

“Tumejizatiti kushirikiana kwa karibu na wadau wa sekta hii kwa kutoa huduma za kifedha zilizobuniwa mahsusi kulingana na mahitaji yao ya kipekee.” alisema Ndyetabura

Zaidi ya washiriki 1,200 walihudhuria mkutano huo, jambo linaloonesha umuhimu na mvuto wa mkutano huu kama jukwaa la majadiliano, ushirikiano na uboreshaji wa uwezo ndani ya sekta ya ujenzi nchini.
Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega (katikati) akimkabidhi cheti Mkuu wa Kitengo cha Biashara kwa Wateja Wakubwa (Commercial Banking) Joyce Ndyetabura (kushoto) cha udhamini wa Mkutano wa Mwaka wa Ushauri wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) kwa mwaka 2025
Wafanyakazi wa Ecobank Tanzania wakiwa kwenye mkutano wa Mwaka wa Ushauri wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB).
Picha ya pamoja
Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Biashara kwa Wateja Wakubwa (Commercial Banking) Ecobank Tanzania Joyce Ndyetabura (kulia) wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Ushauri wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) kwa mwaka 2025.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...