Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO) imekabidhiwa rasmi mradi wa kuunganisha umeme katika vitongoji 105 Mkoani Mbeya, Mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 10.9 kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ambao unatarajiwa kunufaisha wateja takribani 3,465.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi huo iliyofanyika leo Kata ya Igawilo jijini Mbeya, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Akson, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali wananchi kupitia Miradi ya mbalimbali ya maendeleo.

Dkt. Akson amebainisha kuwa tangu mradi wa REA uanze mwaka 2021/ 2022 Serikali imetenga kiasi cha Billioni 71 kwaajili ya kupeleka umeme vijijini kwa Mkoa wa Mbeya, huku akimtaka Mkandarasi wa Mradi ETDCO kuhakikisha anakamilisha Mradi huo kwa wakati ili wananchi wa Mbeya waweze kunufaika na Nishati hiyo ya umeme.

“Nchi yetu ina umeme wa kutosha kutokana na Mradi mkubwa wa Bwala la Mwalimu Julius Nyerere, hivyo Mradi huu wa usambazaji wa umeme kwenye vitongoji 105 unatakiwa kutelezwa kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika na Nishati hii ya Umeme", amesema Dkt. Akson.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka ETDCO, Mhandisi Dismas Massawe, amesema kuwa Kampuni yao iko tayari kutekeleza Mradi huo kwa weledi na kwa wakati kama ilivyo anishwa kwenye Mkataba ili wananchi hao waweze kupata Nishati ya umeme kwa wakati uliopagwa.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu, amewataka wananchi wa Mbeya kujitayarisha kwa kuweka miundombinu ya kupokea huduma ya umeme katika makazi yao ili waweze kunufaika ipasavyo na mradi huo.

Wananchi wa Mkoa wa Mbeya wameipongeza Serikali kwa Mradi huo, huku wakisema kuwa utaongeza fursa za kiuchumi kupitia shughuli zinazohitaji Nishati ya Umeme, ikiwemo biashara ndogo ndogo, kilimo cha kisasa na usindikaji wa mazao.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...