Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa Africa Technology uliofungwa jana Mei 28, 2025.
Rais wa Jumuiya ya Kimataifa Wahandisi wa Petroli Society of Petroleum Engineers International (SPEI)), Olivier Houze akizungumza jana wakati wa kufunga mkutano wa Afica Technology..jpeg)
.jpeg)
Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Dkt. Riverson Oppong akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa Africa Technology uliofungwa jana Mei 28, 2025.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mhandisi Charles Sangweni, akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa Africa Technology uliofungwa jana Mei 28, 2025.
Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyakazi wa Petroli (SPEI) Tanzania, Alex Buko akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa Africa Technology uliofungwa jana Mei 28, 2025.
TANZANIA imepiga hatua kubwa katika sekta ya nishati baada ya kugundua gesi asilia yenye ukubwa wa futi za ujazo trilioni 57.54. Ugunduzi huu mkubwa unatarajiwa kuwa chachu ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa umeme, nishati safi ya kupikia, matumizi viwandani pamoja na kwenye usafiri.
Akizungumza jijini Dar es Salaam tarehe 28 Mei 2025, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, alieleza kuwa gesi hiyo itakuwa kichocheo kikuu katika mageuzi ya kiuchumi kupitia matumizi ya nishati safi na endelevu. Kauli hiyo aliitoa wakati wa kufunga Mkutano wa Africa Technology, uliojumuisha wakurugenzi wa petroli kutoka mataifa mbalimbali pamoja na wanafunzi wanaosomea masuala ya mafuta na gesi.
Mhandisi Luoga alifafanua kuwa mkutano huo ulikuwa ni matokeo ya moja kwa moja ya ugunduzi wa gesi nchini, ambapo serikali imeona umuhimu wa kuwahusisha wataalamu wa ndani kwa kushirikiana na wenzao kutoka mataifa mengine. Lengo ni kubadilishana uzoefu na kujifunza teknolojia za kisasa zinazotumika duniani katika sekta ya mafuta na gesi.
Aidha, Kamishna huyo alisema kuwa kongamano hilo litaharakisha utekelezaji wa mikakati ya serikali katika ujenzi wa miundombinu ya gesi kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Dar es Salaam. Uwekezaji huu utasaidia kufikia malengo ya kitaifa ya usambazaji wa gesi na kuongeza upatikanaji wa nishati safi kwa matumizi ya nyumbani, viwandani na katika magari.
Mhandisi Luoga aliongeza kuwa taasisi zinazohusika na mafuta na gesi zinaendelea na utafiti wa kina katika maeneo ya nchi kavu na baharini, ambapo dalili zinaonesha uwepo wa kiasi kingine kikubwa cha gesi. Hii inaashiria mustakabali mzuri wa nchi kuelekea kwenye uchumi wa gesi.
Kupitia kongamano hili, Tanzania inalenga kuharakisha Mikakati yake ambayo imewekwa kuhakikisha matumizi ya gesi yanaondoa changamoto za nishati nchini huku yakichochea ukuaji wa viwanda na kuimarisha mazingira rafiki kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Bila shaka, ugunduzi huu ni hatua muhimu katika safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa viwanda unaotegemea nishati safi, ya uhakika na endelevu.
Kwa upande wa Rais wa Jumuiya ya Kimataifa Wahandisi wa Petroli Society of Petroleum Engineers International (SPEI)), Olivier Houze amesema kuwa taasisi ya wahandisi wa petroli inawanachama 67,000 duniani kote hivyo "Lengo letu ni dhahiri kukuza ujuzi wa kiufundi wenye mizizi ya Kiafrika na kuibua suluhisho za ndani kwa changamoto katika mafuta, gesi na nishati mbadala."
Alisema kuwa Afrika inakua kwa kasi, na tukio hili limeonesha kuwa wanaweza kwa kushirikiana, kubadilishana maarifa, na kuwekeza katika kizazi kipya cha wataalamu.
Houze alieeleza kuwa Kutokana na mijadala ya kitaalamu hadi ushiriki wa nchi mbalimbali, mafanikio ya mkutano huu ni makubwa na ."Tunatangaza kuwa mkutano ujao wa Africa Technology utafanyika nchini Senegal na baadaye huenda ikazunguka Misri au Afrika Kaskazini tuna matumaini kuwa tutaweza kurudi tena Tanzania tukiwa na mafanikio zaidi." Alieleza Houze
Amesema Afrika inakabiliwa na changamoto nyingi za mabadiliko ya tabianchi na upatikanaji wa nishati nafuu. Lakini hii ni pia ni fursa.
"Ni wakati wetu sasa wa kushiriki kikamilifu kama viongozi, wataalamu, na raia wa bara hili."
Matukio Mbalimbali.
Picha ya pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...