Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Na Kadama Malunde – Malunde 1 Blog

Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga yamefanyika leo ambapo jumla ya wahitimu 147, wanaume 82 na wanawake 65 ,wamehitimu Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Tatu (III) katika fani mbalimbali za Umeme (Electrical Installation), Bomba (Plumbing and Pipe Fitting), Ujenzi (Masonry and Bricklaying), Uhazili na TEHAMA (Secretarial and Computer Application) na Ufundi wa Mitambo Mikubwa (Heavy Duty Equipment Mechanics).

Mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliyofanyika leo Ijumaa Mei 16,2025 alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro.

Akizungumza, Kitinga amewataka wahitimu hao kujisajili katika vikundi ili kunufaika na mikopo ya halmashauri, akisisitiza kuwa fedha zipo kwa ajili yao.“Wanafunzi wanaosoma chuo wapewe mafunzo ya namna ya kusajili vikundi na waunde vikundi ili kupata fedha za mikopo inayotolewa katika halmashauri. Pesa ipo Halmashauri! Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi, kazi ni kwenu kujiunga kwenye vikundi,” amesema Kitinga.

Aidha, amewataka wazazi na walezi kuendelea kupeleka watoto wao VETA ili wapate ujuzi, akibainisha kuwa hakuna kozi za wanaume au wanawake pekee, kwani fursa zinatolewa kwa usawa kwa wote.
Kitinga amewahimiza wahitimu na vijana kwa ujumla kuwa mstari wa mbele katika kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani, huku akiwataka kuwakataa wale wanaohubiri siasa za chuki na mgawanyiko.

“Nchi hii ni tulivu chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Tuilinde amani yetu, tusikubali kugawanywa kwa misingi ya kisiasa,” amesisitiza.

VETA Yazidi Kuandaa Nguvu Kazi Yenye Ujuzi

Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Mwl. Abraham Richard Mbughuni, amesema kuwa chuo hicho kimeendelea kutekeleza dira, dhima na malengo ya mamlaka hiyo kila mwaka.

Tangu kuanzishwa kwake, chuo kimeweza kudahili na kutoa wahitimu wengi wa kozi za muda mrefu, ambao wamejiajiri, wameajiri wenzao au wameajiriwa kwenye taasisi mbalimbali za umma na binafsi.

“Kufuatia maagizo ya serikali, VETA Shinyanga kimefanikiwa kusajili mafundi wapatao 1,553 waliopata ujuzi nje ya mfumo rasmi katika mkoa wa Shinyanga. Lengo ni kuwatambua rasmi, kuwafanyia tathmini na kuwapatia vyeti,” amesema Mwl. Mbughuni.

Aidha, ametumia fursa hiyo kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha VETA, akisema taasisi hiyo ni msingi wa mageuzi ya uchumi kupitia ujuzi.
Mafanikio na Changamoto Chuoni

Msajili wa VETA Shinyanga, Rashid Hamis Ntahigiye, akisoma taarifa kuhusu mafunzo katika chuo hicho, amesema kwa sasa chuo kina jumla ya wanafunzi 575 wa kozi ndefu—wavulana 378 na wasichana 197. Kwa upande wa kozi fupi, wanafunzi waliodahiliwa kuanzia Januari 2024 hadi leo ni 887.

Akitaja mafanikio, amesema kuwa wahitimu wengi wamefanikiwa kupata ajira au kuanzisha biashara binafsi.

Hata hivyo, changamoto kadhaa zinaendelea kukikabili chuo, zikiwemo: Ukosefu wa kituo maalum cha afya kwa ajili ya wanachuo, Uchakavu u wa vifaa vya TEHAMA (kompyuta na mitambo), Uharibifu wa uzio wa chuo na ukosefu wa usafiri wa uhakika kwa jumuia ya chuo.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga yaliyofanyika leo Mei 16,2025- Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Mwl. Abraham Richard Mbughuni akizungumza kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Msajili wa VETA Shinyanga, Rashid Hamis Ntahigiye, akisoma taarifa kuhusu mafunzo katika chuo hicho kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Msajili wa VETA Shinyanga, Rashid Hamis Ntahigiye, akisoma taarifa kuhusu mafunzo katika chuo hicho kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Wahitimu wakisoma risala kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Wahitihimu wakiingia ukumbini kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Wahitihimu wakicheza wakati wa Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Kambi ya Nyani wakitoa burudani kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

MC Manyama akizungumza kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Sehemu ya wahitimu wakifuatilia matukio kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Sehemu ya wazazi na wageni waalikwa wakifuatilia matukio kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Sehemu ya wahitimu wakifuatilia matukio kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Wafanyakazi wa VETA wakifuatilia matukio kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akiwa katika Karakana ya Ukataji Madini Vito katika Chuo cha VETA Shinyanga.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akiwa katika Karakana ya ubunifu, ushonaji na teknolojia ya nguo

Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akiwa katika Karakana ya ubunifu, ushonaji na teknolojia ya nguo

Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akiwa katika Karakana ya umeme

Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akiwa katika Karakana ya umeme

Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akiwa katika moja ya majengo yaliyojengwa na wanachuo cha VETA Shinyanga

Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akiwa katika chumba kinachotoa Fani ya saluni
na urembo

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...