Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Twaha Mpembenwe amesema kuwa, maboresho ya Mahakama ya Tanzania yaliyofanyika yana mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa.

Mpembenwe ameyasema hayo jijini Dodoma,katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma wakati wa Semina iliyotolewa kwa wajumbe (Wabunge) wa Kamati hiyo ya kujifunza kuhusu maboresho mbalimbali ya Mahakama nchini.

Amesema kwamba, Kamati hiyo inaelewa kwamba mashauri yanaposikilizwa kwa wakati na haki inapokuwa imetendeka ina faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuokoa muda ambapo amesema kuwa, muda ni sehemu muhimu katika kukuza uchumi wa nchi.

Amefafanua kuwa,ana imani kuwa mbeleni zaidi, mashauri yatakavyoendelea kusikilizwa na kutolewa uamuzi kwa muda mfupi itaendelea kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

Hata hivyo ameupongeza uongozi wa Mahakama ya Tanzania chini ya Jaji Mkuu kwa maboresho ya miundombinu ya majengo ambayo Mahakama imejenga na inaendelea kujenga, huku akitoa mfano wa Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania kutumika kama kivutio cha utalii.

Amesema kuwa, Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ni utajiri katika nchi katika kuchochea uchumi kwa kuwa watu mbalimbali wanaokuja kujifunza wanachangia kukuza uchumi kupitia hoteli wanazofikia, chakula wanachokula na kadhalika.

“Napenda nikupongeze Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Ole na uongozi mzima kwa maboresho ambayo yanaendelea kufanyika ndani ya Mahakama, ni matarajio ya Kamati yetu na Bunge kwa ujumla kuona mambo makubwa na mazuri zaidi kuendelea kupatikana ndani ya Mhimili huu,” amesisitiza Mhe. Mpembenwe.

Akiwasilisha mada kuhusu Maboresho ya Miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel ameishukuru Kamati ya Bajeti na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano wa karibu ulioiwezesha Mahakama kupata mafanikio kadhaa ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi katika shughuli za Mahakama kutokana na matumizi ya teknolojia.

Prof. Ole Gabriel amewaeleza Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa, Mahakama imefanikiwa kuanzisha mifumo mbalimbali ya TEHAMA ikiwemo Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Mashauri (JoT e-CMS); Mfumo wa Unukuzi na Tafsiri Mwenendo wa Mashauri (TTS); Mfumo wa Takwimu (Data Hub); Mfumo wa taarifa za Hukumu na Sheria Tanzania (TAnzLII); na mingine.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...