Na Janeth Raphael MichuziTv -Bungeni -Dodoma
Mbunge wa Korogwe Vijijini, Timotheo Mzava (CCM) ameiomba Wizara ya Ujenzi kuharakisha mchakato wa ujenzi wa barabara nne za Handeni- Kibrash - Kwamtoro, Tanga- Pangani- Makurunge, Soni- Bumbuli- Dindira -Korogwe na Old Korogwe - Magoma- Mashewa- Bombomtoni na Mabokweni kwani ni muhimu kiuchumi kwa wananchi wa Jimbo hilo.
Akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi katika bajeti ya Wizara ya Ujenzi bungeni kwa mwaka 2025-2026 leo Mei 6,2025,Mzava amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Ulega kwa utendaji kazi mzuri.
Akiizungumzia barabara ya Handeni -Kibrash- Kwamtoro amesema ni muhimu kwa uchumi wa watu wa Tanga ambapo wameomba maelekezo ya Rais yafanyiwe kazi.
"Haya ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais nakuomba sana Mheshimiwa Waziri hii barabara ni muhimu, " amesema Mzava.
Kuhusu barabara ya Tanga- Pangani Makurunge amedai ni muhimu katika kukuza utalii wa Saadan hivyo Serikali ni lazima iingalie kwa umakini.
Mzava pia amesema Wizara iiangalie barabara ya Soni- Bumbuli- Dindira -Korogwe kwa kuhakikisha mkandarasi anaongeza kasi ili barabara ikamilike kwa wakati.
Kuhusu barabara ya Old Korogwe - Magoma- Mashewa- Bombomtoni na Mabokweni amedai ni maelekezo ya Rais Samia ambapo amedai ahadi ni deni hivyo lazima waijenge haraka na kwa viwango

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...