Na Philomena Mbirika, Dodoma

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imetumia fursa ya maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani yanayofanyika jijini Dodoma kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana katika Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

Maadhimisho hayo yaliyoanza Mei 17 na kuhitimishwa leo Mei 20, 2025 katika Viwanja vya Chinangali Park Dodoma Mgeni rasmi akiwa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, yamewakutanisha wadau wa sekta ya nyuki kutoka Mikoa mbalimbali nchini kujadili maswala yanayohusu sekta ya ufugaji nyuki katika uhifadhi na kuleta maendeleo endelevu kwa jamii.

Katika maadhimisho hayo NCAA imepata fursa ya kutangaza vivutio vyake vya utalii vikiwemo Bonde la kreta ya Ngorongoro lenye muonekano wa pekee, wanyama mbalimbali ikowemo wa wanyama wakubwa watano “The big Five “, Laitoli zinakopatikana Nyayo za binadamu wa kale aliyeishi miaka milioni 3.7 iliyopita, Olduvai George eneo lenye gunduzi za kihistoria ya akiolojia, Kreta ya Empakai iliyopambwa na ndege aina ya Flamingo, Tambarare za Ndutu, Kreta ya Olmoti, Jabali la Nasera (Nasera Rock”, Pango la Olkarien, Mchanga unaohama na vivutio vingine.

Akizungumza ndani ya Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye maadhimisho hayo Afisa wa Uhifadhi- Utalii Joseph Mzaga amesema kwamba maadhimisho haya yamewakutanisha na taasisi mbalimbali pamoja na watu binafsi ambao wameza kuwaeleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na NCAA kwenye Utalii, Uhifadhi na maendeleo ya jamii.

“Maadhimisho haya yametupa fursa ya pekee ya kutangaza vivutio vilivyopo ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa watu mbalimbali zikiwemo taasisi, watu binafsi na makundi ya wanafunzi walioweza kukutembelea mahali hapa ambapo wameonesha shauku kubwa ya kwenda kutembelea vivutio hivi” Alisema Joseph

Katika kuelekea Mkutano wa 50 wa Kimataifa wa Shirikisho la Umoja wa Vyama vya Wafugaji nyuki Duniani (Apimondia 2027) unaotarajiwa kufanyika Tanzania, NCAA imejipanga kuonesha utajiri wa rasilimali za asili, utalii wa kipekee na jitihada za uhifadhi kupitia sekta ya nyuki na utalii.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...