Maelekezo yametolewa kwa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS)Mkoa wa Dodoma ambao unasimamia Mradi wa upanuzi wa daraja la Morena, kutafuta njia mbadala itakayotumiwa na wananchi watakaohitaji huduma upande wa pili wa daraja baada ya barabara iliyokua ikiunganishwa na daraja hilo kufungwa kwa muda ili kupisha ujenzi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ametoa maelekezo hayo wiki iliyopita Aprili 29, 2025 alipofanya ziara fupi ya kutembelea eneo hilo la mradi lililopo kwenye makutano ya barabara ya kuelekea Morena na Mkoa wa Morogoro (Shabiby) ili kujionea maendeleo ya ujenzi huo.
“Hapa mmepata mawazo ya kutafuta sehemu nyingine ambazo zinaweza kuwa ‘altenative’, muiwekee vibao ili mtu aone ana ‘option’ tofauti tofauti za kufika katika hilo eneo. Hilo lifanyeni, tarehe 1 tupate taarifa kuwa hawa wananchi wanapita wapi maeneo mengine ili kulifikia hili eneo”.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri amepongeza upanuzi wa daraja hilo kwani utamaliza changamoto ya mafuriko kwenye makazi ya watu kipindi cha mvua kubwa lakini pia litaondoa changamoto za kiafya kutokana na kuzaliana kwa mbu pindi maji ya mvua yanapotuama eneo hilo sambamba na magonjwa ya mlipuko.
Aidha, akitoa taarifa ya Mradi kwa Mhe. Senyamule, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dodoma Mhandisi Zuhura Amani, amesema utekelezaji wa Mradi huo umefikia 80% huku akitoa ahadi kwa wananchi kuwa pamoja na kuzingatia ubora, wataendelea kumhimiza Mkandarasi kukamilisha kazi hiyo mapema ili wananchi waone matunda yake.
Mradi huo ambao umefadhiliwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya shilingi 1.5 unatarajiwa kukamilika Novemba 2025 na kwa sasa Mkandarasi amemaliza ujenzi wa daraja kubwa pamoja na makalavati madogo. Ujenzi wa barabara unganishi unatarajiwa kuendelea ndani ya siku 14 huku ukizalisha ajira 40 kwa wazawa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...