Mwamvua Mwinyi, Pwani Mei 1,2025

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuwa kielelezo cha uongozi bora kwa vitendo, akionyesha njia ya utendaji kazi wenye weledi, jambo ambalo linapaswa kuigwa na watumishi wengine wa umma.

Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi), Kunenge alisema , Rais Samia amekuwa mstari wa mbele kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili wananchi. 

Alieleza, ni wajibu wa wafanyakazi wote nchini kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa kero zinazowakabili wanajamii.

Aidha Kunenge alifafanua, ndani ya kipindi cha miaka mitano iliyopita, Mkoa wa Pwani umepokea zaidi ya shilingi trilioni 1.53 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali.

Kuhusu uwekezaji, Kunenge alisema Mkoa wa Pwani unaongoza kitaifa kwa kuwa na zaidi ya viwanda 1,500, hali ambayo imeongeza fursa za ajira kwa wakazi wa mkoa huo.

Alieleza kuwa kwa sasa mkoa umeanza mazungumzo na wawekezaji ili kuhakikisha wafanyakazi wanapatiwa mikataba ya ajira pamoja na kuchangia katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

Katika hatua nyingine, Kunenge alizitaka taasisi zote zilizotajwa kwenye risala ya wafanyakazi kuwasilisha majibu ya changamoto zilizobainishwa ndani ya wiki moja.

“Kama mikataba haipo, basi tujue ni nani anayehusika, Ninachotaka kuona ni mikataba kuwepo na kila kero iliyoelezwa hapa iwe imepatiwa majibu,” alisema.

Aliziasa sekta zote – binafsi na za umma – kuongeza bidii katika kazi, kuongeza mapato, na kujikita katika ushindani wa mafanikio kama ambavyo Rais Samia haamini katika kushindwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TUCTA Mkoa wa Pwani, Ramadhan Kinyogori, alimshukuru Rais Samia kwa juhudi zake za kutatua changamoto za wafanyakazi nchini.

Awali, Mratibu wa TUCTA Mkoa wa Pwani, Susan Shesha, akisoma risala ya wafanyakazi, aliipongeza Serikali kwa kuwa sikivu na kuanza kutekeleza maazimio ya mabaraza ya wafanyakazi katika wilaya zote za mkoa huo, hali iliyowezesha utoaji wa huduma bora mahala pa kazi.

Shesha alitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili wafanyakazi kuwa ni pamoja na mishahara midogo isiyoendana na hali halisi ya maisha, pamoja na baadhi ya waajiri kutotoa mikataba ya ajira, kuwazuia wafanyakazi kushiriki sherehe za Mei Mosi, na kushindwa kuchangia mifuko ya hifadhi ya jamii.

Mratibu huyo alitoa wito kwa waajiri kutimiza wajibu wao kwa wakati, hususan katika ulipaji wa madeni, ili kuepusha migogoro ya kikazi.

Mtumishi wa kitengo cha habari ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani ambae amepata tuzo ya mfanyakazi bora, Nasra Mondwe alishukuru na kusema imempa morali wa kufanya kazi na kujituma kwa bidii. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...